Tambua asali halisi kwa njia hii rahisi kabisa popote utakapokuepo

Tambua asali halisi kwa njia hii rahisi kabisa popote utakapokuepo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
1463399_249850455169877_1260361916_n.jpg




Matumizi ya asali ni mazuri kwa afya yako lakini ikiwa tu utatumia ASALI HALISI na sio asali ILIYO CHAKACHULIWA. Ukitumia asali halisi utapata matokeo unayoyategemea na si vinginevyo.

Kutambua asali halisi fata mtiririko huu:-

1.Chukua glass unayoweza ona ndani kwa urahisi.

2.Jaza maji angalau nusu

3.Dondoshea asali taratibu kwenye glass yenye maji kama inavyoonekana kwenye picha.

4.Asali halisi inatakiwa iende mpaka chini na kutulia na isijichanganye na maji. Kama asali uliyonayo sio halisi pindi itakapogusa maji tu itajichanganya na maji hayo.

N.B
Epuka kutapeliwa eeh ndugu yangu.

 
Umeeleweka mkuu.Vp kuhusu maziwa yalochakachuliwa? Kuna njia yoyote yakuyatambua?
 
dondosha tone la asali halisi katika kipande cha karatasi au gazeti hakiwezi kuloana kirahisi lakini asali fake iliyozimuliwa na maji gazeti litalowa haraka.
 
Tunashukuru kwa elimu tuliopata, kama alivyosema mwenzetu, je na maziwa yaliyochakachuliwa inawezekana?
 
Kwa mie mtumia asali huwa Napata wakati mgumu sana kutambua hii, asante kwa kunifunza.
 
mpo sahihi wote, mim dealer wa asali zote, ya nyuki wa pole na wakali, rejareja na jumla. muhitaji tuwasiliane kupitia 0766979850

Pamoja na kudandia uzi wa mwenzako kuwela tangazo lako,jitahidi ukamilishe Tangazo weka items za msingi, mfano Bei kwa lita, mahali ulipo, na mambo kama hayo!
 
Pamoja na kudandia uzi wa mwenzako kuwela tangazo lako,jitahidi ukamilishe Tangazo weka items za msingi, mfano Bei kwa lita, mahali ulipo, na mambo kama hayo!

Kaweka namba ya simu kwa anayetaka kujua hivyo vyote!!!
 
Back
Top Bottom