Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Ukiwa kwenye mahusiano yoyote lengo lako liwe ni kukua katika kila nyanja zaidi ya jana.
Kukua kimwili (je uliyenaye anakusaidiaje kuwa na afya bora zaidi?), kiakili (je, uliyenaye anakupa changamoto gani za kufikiri ili kukua?) na kiroho (je, uliyenaye anamachango gani kwenye safari yako ya kiroho?). hivyo hakikisha mahusiano unayotengeneza na rafiki yako, boss wako, mtoto wako au mpenzi wako hakikisha yanakusaidia kukua.
.
Ili mahusiano yakusaidie kukua ni vizuri pia na wewe umsaidie huyo mwenzako kukua (kiakili, kimwili na kiroho). Njia nzuri ya kufanya hivyo ni kujitoa kwa moyo kwenye hayo mahusiano na kuhakikisha mahitaji ya mwenzio yanafanikishwa.
.
Jitoe kumsaidia mwingine bila kujali sana nini utapata toka kwake, usiwe kwenye mahusiano ukifikiria natakiwa nipate kitu. Lakini ni muhimu kujilinda ili usijitoe sehemu ambayo siyo sahihi. Utaumia.
Ili kujilinda hakikisha mtu uliyenaye pia ni mtu wa kujitoa kwenye hayo mahusiano yenu ili kukufanikishia mahitaji yako pia. Hivyo, sio kwasababu inabidi ujitoe kwa moyo ndo uwe na mtu anayechukua tu kutoka kwako na kukunyonya/ kukunyanyasa, hapana una uwezo wa kuachana naye na kuamua vingine sababu unastahili kupata furaha kwenye mahusiano.
.
Heri utafute ndege utakayefanana naye na mruke pamoja.
Niwatakie Jumapili Njema yenye Heri