EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Kwa nini kumekuwa na hii tabia ya kila mfanyabiashara anajiita mjasiliamali? Labda tunashindwa kutofautisha haya maneno mawili ndiyo maana yamekuwa yakituchanganya na hasa walio wengi. Huwa nakasirika sana napoona mtu anatumia neno au kitu bila kujua maana yake na huku kukasirika kwangu ni kwa kibinaadamu tu. Ila papo hapo huwa najiuliza mwenyewe kwanini nakasirika labda aliyekuwa analitumi labda anayelitumia hili neon hajui maana yake na kama hajui maana yake kwanini analitumia?.
Basi majibu huwa ni kwenye kuelimishan ili kuweza kujiwekana sawa kwenye hili jambo. Na kuelemishana huku natumaini kutaleta mabadiliko makubwa na makosa hayataweza kurudiwa tena na hata kama ikitokea yamerudiwa inakuwa ni rahisi kumuelekeza/kumuongoza mtu pale atakapoweza kusoma na kurekebisha makosa yake. Kwa kifupi nitajitahidi kutoa muongozo kadri ya nafasi na muda wangu unavyoniruhusu.
Kwakuwa mjasiliamali na mmiliki/mfanya biashara wote ni wadau kwenye biashara na hapa ndipo mkanganyiko wote unapotokea. Hivyo ni vizuri tuchambue utofauti wa maneno haya mawili ya ujasiliamali (entrepreneurship) na umiliki/mfanya biashara (proprietorship) halafu ndiyo tutapata fursa ya kujua tofauti halisi. Hivyo naamini kama tukiweza kupata umaana kamili wa ujasiliamali basi tutaweza kutambua utofauti wake na neno mmiliki/mfanya biashara.
Ujasiliamali (entrepreneurship) unatokana na neno la Kifaransa entreprendre lenye maana ya kufanya kwa kiswahili. Kwenye hali/mazingira ya kibiashara na uhasilia wake hivyo neno hilo lin maana ya kufanya biashara. Hivyo tunaona neno ujasiliamali linavyoshahabiana na mmiliki/mfanya biashara kwa kiasi kikubwa. Ila pia kuna tofauti kubwa ya kwenye matumizi ya haya maneno kutokana na mazingira ya biashara yanayoyazunguka. Kwa maana nyingine ni kwamba siyo kila mfanya biashara ni mjasiliamali.
Hivyo ni vema tukaona ni vipi haya maneno yanatafsiriwa na watu wenye weredi wa maswala ya biashara au mambo yenye mahusiano na biashara. Katika miaka ya 1800, mchumi wa kifaransa , J.B Say alisema "ujasiliamali ni madiliko ya rasilimali za kiuchumi kutoka kwenye kiwango cha chini cha uzalishaji na kwenda kwenye kiwango cha juu na mavuno makubwa". Wasomi wa Kiingereza Stokes, Wilsons na Mador wao walisema ujasiliamali unahusisha utengenezaji wa thamani kupitia mafanyiko ya uvumbuzi kwenye masoko ya kibiashara. Hapa sasa tunaona neno uvumbuzi maana yake kitu kipya kwenye soko la kibiashara.
Lakini, pia profesa wa kimarekani kwenye ujasiliamali, alisema " ujasiliamali ni nguvu ya mchakato yenye maono, mabadiliko, kujenga ambayo inahitaji nguvu, shauku kwenye uundaji na utekelezaji wa mawazo mapya ya ubunifu na uvumbuzi. Haya maneno niliyoyawekea mkazo hapo juu ndiyo yanayoleta maana nzima ya ujasiliamamli na utafauti kwenye mazingira ya kibiashara.
Pia utofauti mkubwa wa mjasiliamali na mmiliki/mfanya biashara unaoneka kwenye maeneo yafuatayo:
1: Kiasi cha faida/thamani kinachotarajiwa au tengenezwa: Lengo la mjasilimali kujiingiza kwenye biashara si kujitafutia nafasi ya kutengeneza kiasi sawa au zaidi kidogo na mshahara wa kawaida. La hasha lengo kuu ni kweza kutengeneza mamilioni mengi ya shilingi au kuridhisha msukumo unaotoka ndani ya mwili wake. Kwa maana hii ndiyo maana mjasiliamali wanakuwa na tabia tofauti sana na mmiliki/mfanya biashara wa kawaida.
2: Muda wa Kutengeneza hiyo faida: mmiliki/mfanya biashara huwa hategemei sana faida ya haraka kama mjasiliamali. Pia kwa mjasiliamali ikiwezekana anaweza hata kuiuza biashara yake kwenye kipindi kifupi tangu kuanzishwa kama ana uhakika wa kutengeneza mamilioni ya shilingi kwenye mauzo.
3: Mjasiliamali hufanya biashara kwenye mazingira hatarishi zaidi kuliko mmiliki/mfanya biashara kwa kutegemea faida kubwa. Hivyo bila hiyo shauku ya ujasiliamali isingekuwepo kwa sababu nani angekuwa yuko tayari kujiweka kwenye mazingira makubwa hatarishi kwa kupata faida au thamani ndogo.
4:Uvumbuzi ni jambo ambalo linahusiana kwa kiasi kikubwa cha ujasiliamali na linaloipa biashara ya mjasiliamali faida za kiushindani ambayo ndiyo inayotengeneza utajiri au mamilioni mengi ya shilingi. Huu uvumbuzi unaweza kuwa kwenye bidhaa,soko, huduma au mchakato mzima wa uendeshaji wa biashara. Mfano: McDonald, baga ni bidhaa ambayo waliivumbua hapana baga zilikuwepo tangu zamani. Ila huduma za ile baga ndiyo ilikuwa ni ya uvumbuzi na mchakato mzima wa uendeshaji. Pia walivumbua soko jipya na wateja wapya kabisa. Mfano mwingine IPP media, radio ilikuwepo tayari Tanzania ila kuleta FM ilikuwa ni uvumbuzi mpya kwenye soko la Tanzania, ikatengeneza soko jipya na wateja wapya.
Sasa Je kwa sisi wadau wa biashara, swali linakuja kwetu kwenye maelezo yangu wewe ni nani kati ya mjasiliamali na mmiliki /mfanya biashara? Je ni sahihi kwa kila mtu kujiiita mjasiliamali? Au kila biashara ni ujasiliamali?