Tambua ugonjwa wa kusahau (Alzheimer's Disease)

Tambua ugonjwa wa kusahau (Alzheimer's Disease)

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2021
Posts
373
Reaction score
627
Chembe hai za ubongo (neuronal cells) zina utando unaoitwa Sphingolipids( Haya ni mafuta maalum ya ubongo) na mojawapo yanaitwa Sphingomyelin.. mafuta haya husaidia kusafirisha taarifa ( impulse) ambayo huwa katika mfumo wa umeme( action potential).Taarifa ya kusikia , kuona , maumivu nk.

Cholesterol pia hutengeneza ukuta wa chembe hai zote za mwili( component of cell membrane of all cells).Kwa hiyo hata kwenye chembe hai za neurone kuna cholesterol kwenye kuta zake.

Kwa hiyo cholesterol na Sphingolipids ni partners kwenye kuta za chembe hai.
Note : Neurone zina kiwango kikubwa cha sphingolipids.

Alzheimer's disease ( kufa kwa chembe hai za ubongo) hutokana na Protein ambayo haijakunjwa,Kitaalamu inaitwa unfolded protein (Amyloid Precursor Protein..APP).

KWA NINI PROTEIN ISIKUNJWE? Protein zote mwilini hukunjwa na kuwekwa kwenye bahasha maalum kisha kupelekwa sehemu husika ili mwili usikonde. Endapo protein haitakunjwa basi chembe hai kwenye eneo hilo hufa (unfolded protein response). Risk kubwa ni kutofanya mazoezi , funga ya muda au ongezeko kubwa la uzito.
Pia sababu za urithi( genetic factors) husababisha protein isikunjwe.

Hizi Amyloids zikirundikana kwenye ubongo kama nilivyoandika ubongo hufa, kwenye moyo husababisha ufeli, kwenye figo lakini pia hata kwenye ngozi.

Wakati fulani niliona/nilishuhudia case ya mgonjwa wa amyloid kwenye ngozi( skin Amyloidosis) ngozi huwa kama plastic, unashangaa ngozi ya jicho imefunikwa.

Kwa kifupi Alzheimer's disease haitokani na hitilafu ya cholesterol bali Amyloid Protein na tafiti zinaonyesha matumizi ya Statin ( dawa za kupunguza cholesterol) huepusha risk za Alzheimer's disease.

Tuendeleeni na mazoezi , ulaji mzuri kuidhibiti cholesterol, kupunguza uzito na funga ya muda.

Kuhusu tiba na dawa ya kuondoa cholesterol na kupunguza uzito nilishaeleza kwa kirefu katika maandiko yangu ya nyuma,unaweza kurejea.

MHIMU: Tupambanie na kutunza afya zetu maana ndiyo nguzo mhimu ya shughuli zetu za kila siku,bila afya imara hakuna fikra imara.
 
Elimu hii tumeipata bure kabisa,uzidishiwe maarifa yako yatunufaishe zaidi
 
kule tiktok kuna jamaa mmoja mzungu huwa anamtengenezea content baba yake mzazi ambaye anasumbuliwa na huo ugonjwa wa kusahau.

baba yake alikuwa afisa mkubwa wa US navy.,baada ya kustaafu ndio akapata

Alzheimer.​


katika moja ya video, anasahau mpaka jina la mwanae aliyemzaa. noma sana aise.
 
kule tiktok kuna jamaa mmoja mzungu huwa anamtengenezea content baba yake mzazi ambaye anasumbuliwa na huo ugonjwa wa kusahau.

baba yake alikuwa afisa mkubwa wa US navy.,baada ya kustaafu ndio akapata

Alzheimer.​


katika moja ya video, anasahau mpaka jina la mwanae aliyemzaa. noma sana aise.
Kwa sasa ni ugonjwa unaoendelea kuwapata watu wengi,kulingana mtindo wa maisha yetu ya kila siku.
 
Back
Top Bottom