Tambua Usawa Uliopo Kati ya Ufahamu, Akili na Uhalisia wa Maisha Yetu

Tambua Usawa Uliopo Kati ya Ufahamu, Akili na Uhalisia wa Maisha Yetu

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240
Kanuni ya Usawa wa Ufahamu, Akili na Uhalisia wa Maisha ya Mtu
"Like attracts Like"






Kanuni hii kwa Upande wa Ndani
Sheria hii wengi wanaifahamu ikisema "Like attract like". Kuelewa sheria hii, kwanza ni vyema kufahamu kuwa Akili imegawanyika katika Subconscious Mind na Conscious Mind. Conscious mind ni sehemu ambayo ndiyo tunaicontrol lakini subconscious mind ni upande ambao ni asilimia kubwa ya akili yetu na ndipo maajabu na nguvu ya akili yetu ilipo. Ni upande ambao hatuwezi kuucontrol directly mpaka kujizoesha au kutumia conscious mind kuiongoza. Ndiyo part inayocontrol vitu au hali bila control yako. Mfano kusimamia kiasi cha sukari mwilini, kubadilisha seli na kutengeneza seli, kuamua ni kiasi gani na aina gani ya hormone kutoka, inaongoza joto la mwili, na kadhalika. Vyote hivi wewe huviongozi lakini sehemu hii inaviongoza bila kuhitaji msaada wako. Ni sehemu ambayo ukijizoesha kitu kupitia akili yako kinaingia kwenye conscious mind (akili ya milango ya ufahamu na yenye kuhusiana na judgements), baada ya kuzoea sana subconscious mind inarecord na kuhifadhi ujuzi, experience na uelewa wake.


  • Mfano ukitaka kujifunza kuendesha gari akili (katika sehemu ya consciousmind) inaanza kujifunza na neurons zinajitengeneza kuweka kumbukumbu ya hiyo experience, halafu taaratibu na subconscious mind inapokea ujuzi huo. Na ndio maana unaweza kuendesha gari akili yako ikiwa kwingine. Pia hata miaka ikipita bila kuendesha gari automaticaly siku ukija kuendesha hautaona ni kigeni kwani kumbukumbu yake ipo kwenye subconscious. Ni experience moja sawa na kuogelea, kujifunza kupiga kifaa cha muziki, na arts.


[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kazi ya conscious mind na subconscious mind.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Hivyo subconscious mind ni kama sehemu inayojaribu kuleta experience ya kilichopo kwenye conscious mind. Unapoamini jambo fulani au unapoweka mtazamo fulani kwenye conscious mind kinajiweka kwenye subconscious mind, na reality, mazoea, experience nayo inajiweka kutokana na kilichopo kwenye ufahamu wako.

Kanuni hii inatusaidia sana kwa kutujulisha kuwa kila experience iliyopo nje yetu imepitia katika ufahamu wetu kwanza. Labda nikuulize kitu, unaweza kuimagine kitu ambacho hujawahi kukiona kabisa wala kupata idea yake kwa kutumia imagination inayojitegemea na uliyoizoea? No, ila unaweza kuimagine kitu kutokana na experience fulani au experience mbalimbali na ukatengeneza picha mpya kutoka katika kilichopo katika ufahamu wako. Hivyo hatuna uwezo wa kuimagine au kutengeneza tusichokifahamu nje ya experience tunayoifahamu bali tunaboresha experience baada ya experience kwa kutengeneza experience nyingine.

Pia kanuni hii inatusaidia kufahamu kuwa hakuna kinachoingia kwenye subconscious mind bila kupitia kwenye conscious mind.

Ulishawahi kufanya kitu unconsciously na ukajikuta unashangaa how uliweza kumanage that? It happen.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Akili ya Mwanadamu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Tazama kanuni hii kwa upande wa Nje.

Like attract like. Kitu cha vibes fulani hukaribisha kitu au hali yenye vibes (vibration) kama yake. Chunguza vizuri hata katika maisha kwa ujumla. Tazama watu wanaokuzunguka, utagundua kuwa watu wenye tabia fulani, maneno fulani au fikra fulani hukutana na experience mbalimbali zenye experience sawa na hisia, tabia, maneno na fikra zao. Huwezi kukuta mtu mwenye maisha tofauti na yanayoendana na yeye alivyo ndani yake. Ulimwengu wako wa ndani ulivyo kwa hivi sasa ndio uhalisia wako ujao unavyojijenga.

Matumizi ya Kanuni Hii
Kutokana na watu fulani kufahamu siri hii wamekuwa wakiweka experience na reality wanayoitaka wao kwa watu bila watu hao kujijua kuwa wanacho-experience ni tofauti na sababu wanayoamini inawafanya wa-experience hawaijui.

Mfano kwa kutumia kurudiarudia (repetition) na kuteka imani ya mtu kunaprogram subconscious za yake. Unaporudia rudia kitu unakipa nafasi kuingia kwenye subconscious mind na kikishaingia kwenye subconscious mind ni vigumu kukiondoa na experience yake inaanza kufanyika kwenye uhalisia unaouishi. Mfano kurudia rudia maneno katika sala kunasaidia kupelekea ufahamu wa ndani kuchukua na kuweka akilini maneno hayo. Na sio tu sala, hata katika maisha ya kawaida mtu akianza kusema jambo fulani na kulirudia rudia huku akiliamini linamkaa katika subconscious na kuexperience reality zinazoendana na anachokiamini kila siku na kujisemea kila siku.

Hata katika nyimbo kwenye maredio ikirudiwa sana automatically utaanza kuielewa na kuipenda, hata matangazo hutumia ujanja huo, hata arts na kadhalika wote hutambua kanuni hii ni huitumia vyema.

Jitambue
Shukuru kwa kila jambo na yatumie maisha kujifunza, kujibadilisha kwa kuwa bora zaidi na kujitambua zaidi. Kushukuru kwa kila jambo ni kama kusurrender kwenye subconscious mind na kuacha ulimwengu ukuletee experience mbalimbali. Unaposhukuru kwa kila jambo unaanza hatua ya kwanza ya mabadiliko ya maisha yako. Ukiweza kuprogram subconscious mind yako katika hali ya kuwa mtu wa kushukuru, itakueletea experience nzuri zaidi za kukufanya ushukuru zaidi kwani umeprogram akili yako na mazoea yako ya kuwa addicted na kushukuru. Ndio maana hata kama upo katika hali gani huwezi kukosa cha kuanza nacho kwa kushukuru, katika kila experience kuna Hasi na Chanya. Unapoweka mtazamo wako kwenye Upande mmoja unaukuza upande huo.
 
Nice presentation
Jaribu kuchimba zaidi ukilinganisha na role of attitude ku scientific, na hisi utaeleweka sana
 
naombamni add kwenye ilo group nama ni
0764411446
 
asante sana kwa elimu hii. nahitaji kujua zaidi naomba umpe mwalimu 0765896940. aniunge katika group.
natanguliza shukrani.
 
asante sana kwa elimu hii. nahitaji kujua zaidi naomba umpe mwalimu 0765896940. aniunge katika group.
natanguliza shukrani.

Kababaa huchelewi ndugu kweli wewe nimuadilifu na mimi nasubiri kuunganishwa nimewasiliana na mwalimu mmoja anasema wanajiandaa ili kuanza mafunzo hivyo nimeambiwa niwe mvumilivu nikisubiri mafunzo
 
Habari ndugu zangu.

Naomba radhi kwa kutoonekana kwa Kanuni ya Mwisho ya Akili na Ulimwengu. Niliiweka hapo jana katika Jamii Forum Inteligence lakini mods mpaka sasa hawajaipita na kuiweka publish. Niliweza kumaliza kuelezea kanuni ya kumi ambayo ilikuwa ni fupi kidogo lakini asilimia kubwa ya mada katika kanuni ya Kumi ina UFUPI wa Kanuni zote 10 za kuzifahamu na kushikilia katika maisha yetu. Pia niliandika mambo ya muhimu kuyafahamu katika kanuni hizo na summary kwa ujumla kwale waliokosa baadhi ya kanuni au kutoelewa vyema watakuwa na mambo ya muhimu kuyafahamu.

Unaweza kusubiria Mods waweze kuipitia au unaweza kusoma kupitia Mwisho wa Kanuni kuu 10 Za Akili na Ulimwengu. (Ujumbe).

Nashukuru sana kwa wale waliochangia na kuweza kuzingatika kanuni hizo, naahidi mtaona mabadiliko makubwa katika utambuzi na umakini kwa ujumla. Tusiache kujifunza na kufahamu mengi kwani ndio njia sahihi katika kufahamu maisha yetu vyema.

Asanteni sana. Kwa maswali na mada mpya ambazo bado zina utata unaweza ukacomment au ukaniPM nikaanda mada na kila mmoja akaisoma na kuongeza utambuzi zaidi.

Mbarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom