Tambwe: Nitailiza Simba nikipangwa

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, yupo kambini na kikosi cha timu hiyo ku- jiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru na amesema kama mambo yataenda sawa na kupata nafasi ya kucheza atawaliza mashabiki wa timu yake hiyo ya zamani.

Kocha msaidizi wa Yanga inayod- haminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, Shadrack Nsajigwa, aliliambia Nipashe jana kuwa, Tambwe na kiungo Thabani Kamusoko wataun- gana na timu hiyo kwenye kambi yao mjini Morogoro leo.

Akizungumza na Nipashe juzi, Tambwe alisema kuwa anashukuru kupona majeraha yake na ana- tamani kucheza kwenye mchezo wa Jumamosi ili kuwapa furaha mashabiki wa timu yake.

“Nipo vizuri, nitaungana na wen- zangu kwenye maandalizi ya mch- ezo dhidi ya Simba, kocha ndiye mwenye uamuzi, lakini binafsi kama nitapata nafasi ya kucheza nitahakikisha naifunga Simba,” alisema Tambwe ambaye amekuwa na bahati ya kuifunga Simba kwe- nye michezo miwili iliyopita.

Mshambuliaji huyo raia wa Bu- rundi hajaichezea timu yake msimu huu kutokana na kuwa majeruhi na kwa sasa yeye pamoja na Kamusoko wameripotiwa kupona majeraha yao.

“Ninashauku ya kuitumikia timu yangu, mpira ni kazi yangu na Yanga ndio mwajiri wangu..., nataka kuona naisaidia timu kutetea ub- ingwa wake msimu huu pamoja na kuwa ligi inaonekana kuwa ngumu zaidi msimu huu,” alisema Tambwe.


Nipashe
 
Kazi imeanza, oyaoya Simba kaeni mkao wa kula jiandaeni kisaikologia kufungwa 1-0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…