Sote tunafahamu kwamba Katibu Mkuu wa TAMISEMI alitangaza majina ya waalimu wapya mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu. Akatoa maelekezo kwa waajiriwa wapya kwenda kuripoti kwenye Halmashauri walizopangiwa kuanzia tarehe 1 hadi 14 Desemba.
Katibu Mkuu huyu alikwenda mbali zaidi na kuwaelekeza Wakurugenzi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa kusimamia kwa karibu suala la kukamilisha taratibu za ajira mapema iwezekanavyo ili waajiriwa hao waingizwe kwenye orodha ya malipo yaani payroll ili kuondoa suala la malimbikizo ya mishahara isiyokuwa na ulazima.
Lakini hayo maagizo hayakutekelezwa ipasavyo kwenye baadhi ya Halmashauri hapa nchini.
1. Wakurugenzi hawajaandikia waajiriwa mpya barua za posting
2. Wakurugenzi hawajawapa waajiriwa fomu za kudai fedha za kujikimu
3. Wakurugenzi hawa wamewaachia Maafisa Utumishi na Utawala kazi ya kusimamia zoezi la ajira ya walimu wapya, Jambo ambalo ni sahihi. Lakini hawasimamii ipasavyo zoezi hilo. Hali hii imesababisha urasimu mkubwa sana.
Yaani wamebakia tu kupokea waajiriwa na kuwapa fomu za ajira. Zaidi ya yote wanadai kuwa hawataweza kuwapa barua za posting, fedha za kujikimu na mishahara ya mwezi disemba.
Kisingizio chao kikubwa ni kwamba wanasubiria uhakiki wa NECTA ukamilike ndo waendelee na taratibu zingine.
Inawezekana sababu zao ni sahihi ila sasa inaweza kuendelea kuleta urasimu mkubwa hata kipindi cha mwezi Januari 2021, walimu hawa wapya wakashindwa kuanza maisha vizuri hali ambayo inaweza kusababisha ufanisi mdogo wa kazi kwa hawa waajiriwa wapya.
Asanteni, naomba kuwasilisha.