LGE2024 Tamisemi iko chini ya rais, CCM ndio chama Tawala ni sahihi mwenyekiti kumuomba waziri aliye chini yake kupuuza makosa madogo madogo ya wagombea?

LGE2024 Tamisemi iko chini ya rais, CCM ndio chama Tawala ni sahihi mwenyekiti kumuomba waziri aliye chini yake kupuuza makosa madogo madogo ya wagombea?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Boi Manda

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2023
Posts
388
Reaction score
506
Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake wamekuwa na utaratibu wa kutengeneza tatizo na kulitatua wao wenyewe ili waonekane wema kwa Wananchi na tasisi za ndani na nje ya nchi

Pia soma

Kitendo cha Katibu mkuu wa CCM Dr. Emmanuel Nchimbi leo kukutana na waandishi wa habari ofisi ndogo Lumumba jijini Darisalama na kusema kwa niaba ya mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni rais wa nchi kuomba waziri wa Tamisemi kupuuzia makosa madomdogo yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni usanii mtupu

Cha kushangaza wizara ya Tamisemi iko chini ya rais maamuzi ya wizara hiyo kukata majina ya wagombea ni maamuzi ya ofisi yake angeweza kupiga simu tu kwa waziri au kumuita ofisini kwake kumuamuru kuacha uhuni huo mara moja

Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kinachoongoza nchi na rais mwenye ofisi yake ya Tamisemi ndio imekata majina ya wagombea leo hii kuomba wasifanye hivyo ni jambo linalofikilisha kwa watu wazima wenye akili zao

Huko kunaitwa ni kutengeneza tatizo halafu unalitatua mwenyewe sawa sawa na baba ndani ya nyumba anaanzisha utata kwa mkewe na watoto wake kisha anautatu baadaye wanamsifu mshua ana akili nyingi sana huyu na huruma kwa familia yake

CCM Comasava
 
Jamani! jamani !jamani ! Tanzania, pole sana mama yetu Tanzania kweli alie tuloga bilashaka alikufa mda mrefu sana.
Kodi za watanzania zinapotea bure kwa kucheza mchezo wa kombolela. Pole sana Tanzania
By mwinjilist wenu Gabeji.
 
Kimsingi ukweli ndio huo.
Uchaguzi kati ya wagombea vyama vya Upinzani na chama tawala, unaratibiwa na kuamriwa na chama tawala.

Kiukweli hakuna uchaguzi hapa. Ni kupotezeana muda tu.
 
Back
Top Bottom