TAMISEMI imulikeni wilaya ya Kilindi inachonganisha wafanyakazi na Serikali

TAMISEMI imulikeni wilaya ya Kilindi inachonganisha wafanyakazi na Serikali

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2014
Posts
744
Reaction score
1,621
Waziri wa Tamisemi Madam Ummy, kama kuna wilaya inayoleta uchonganishi katika mkoa wa Tanga kati ya wafanyakazi na serikali yao basi ni wakuu wa idara ya wilaya ya Kilindi.

1. Wakuu wa shule wanalazimishwa kutoa pesa kwa kila mihutasari wanayopitisha, yaani lazima utoe kitu kidogo ili muhtsari upite,

2. Wakuu wa shule wanalazimishwa kumega posho yao kila mwezi kuwapa wakubwa hao, na mkuu wa shule anayekataa kutoa mzigo anasimangwa au kutishiwa kuondolewa na kwa ajili ya kuficha uozo huu, mkuu mmoja wa shule jina X anakusanya pesa hizo kwa namba ya VODA na kisha anawasilisha mzigo huo kwa wakuu.

3. Nauli za likizo tangu 2017, 2018 na 2019 mpaka leo kuna watumishi hawajalipwa, na ili kulipwa mpaka mtumishi utoe hongo , imagine mtumishi anadai laki 3 nauli lakini anatakiwa kutoa pesa ili alipwe nauli yake?

4. Wizi wa mitihani, bado halmashauri hii haijaacha huu utopolo pamoja na kupigwa mkwara lakini bado kuna shule zinafanya hii kitu

Najua waziri Ummy ni mchapakazi na tuhuma hizi hazitapita bure.
 
Back
Top Bottom