Walimu waliofanya kazi ya kusahihisha Mtihani wa Kidato cha Nne Kanda ya Nyanda za Juu mwezi Julai mwaka 2022 hawajalipwa pesa yao hadi leo na wamekuwa wakipewa ahadi hewa na bosi wao ambaye ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Katavi.
TAMISEMI wasaidieni walimu walipwe haki yao maana inaonekana kama bosi huyo hajali yuko bize na mambo yake binafsi na pengine pesa imeshaliwa.
Pesa ilichangwa kutoka shule zote za sekondari tangu Julai hadi sasa walimu wanazungushwa tu na hakuna sababu yoyote ya kueleweka wamepewa.
Suala hili naamini Mkuu wa Mkoa anajua lakini sijajua kwanini kakaa kimya.
Mnasema mnawajali walimu sasa mbona wanadhulumiwa na mko kimya? Fuatilinieni suala hili linavunja ari ya walimu kufanya kazi.
Mikoa mingine yote wamelipwa siku nyingi siku nyingi isipokuwa Katavi tu.