Pre GE2025 TAMISEMI iweke utaratibu maalumu wa Ubandikaji wa Mabango kwa Wagombea kuepusha ubandikaji holela na Uchafuzi wa mazingira

Pre GE2025 TAMISEMI iweke utaratibu maalumu wa Ubandikaji wa Mabango kwa Wagombea kuepusha ubandikaji holela na Uchafuzi wa mazingira

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Tanzania inaelekea kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024. Kwa sasa joto la uchaguzi huo limezidi kupanbda na Wagombea wengi wapo kwenye hatua za kurejesha fomu zao ili kupitishwa kugombea nafasi walizokusudia.

Imekuwa kawaida kwa Chaguzi zilizopita kupita nje ya nyumba yako kukuta mlango wako na miti imebandikwa picha za Wagombea wa Vyama mbalimbali ili kuwashawishi watu wawapigie kura.

Usiombe uwe una geti kubwa, Wagombea wa vyama mbalimbali watalitumia kama bango la matangazo kwa kuweka vipeperushi vinavyowatangaza.

Tabia hii inafanyika kwenye miti, nguzo za umeme, vibanda vya biashara, maeneo ya vituo vya usafiri.

Napendekeza TAMISEMI waweke kanuni au sheria inayotoa muongozo kwa Wagombea kuwa na mipaka katika kubandika matangazo yao ili kuepusha kero na uchafuzi wa mazingira unaofanywa.

Ahsante

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Mwanasiasa atakayebandika Mabango ya Kampeni ayaondoe Uchaguzi Ukiisha ili Kulinda Mazingira yetu
 
Mtu akibandika mtangazo wake wa kijani kwangu nampopoa na manati
 
Back
Top Bottom