LGE2024 TAMISEMI: Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2024 zitaanza tarehe 20 hadi 26, Novemba

LGE2024 TAMISEMI: Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2024 zitaanza tarehe 20 hadi 26, Novemba

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

OR TAMISEMI

Ministry
Joined
Jul 3, 2024
Posts
20
Reaction score
93
95d64300-7f32-453b-92a1-0fed602f2daa.jpeg



View: https://www.youtube.com/watch?v=-XzJJFDbKNc

========​


Kipenga cha uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2024, kitapulizwa leo Alhamisi, Agosti 15, 2024 wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa atapotoa tangazo la uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah, tangazo hilo litatolewa viwanja vya Chinangali jijini Dodoma saa 5 asubuhi.

“Tangazo hili litakwenda kutoa maelezo mbalimbali ya namna ya uchaguzi utakaofanyika na mtiririko mzima wa matukio ya uchaguzi wa Serikali za mitaa,” amesema Hosseah.

Miongoni mwa yatakayobainishwa ni pamoja na kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji katika mamlaka ya miji midogo za mwaka 2024, na kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa, 2024.

Nyingine ni kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mamlaka ya wilaya, 2024 na kanuni za uchaguzi wa Serikali katika mamlaka za miji.

Kanuni hizo zinampa mamlaka waziri husika kutoa tangazo kwa umma kuhusu kuwapo kwa uchaguzi katika magazeti ya Kiswahili na Kingereza yanayosambazwa nchi nzima, na katika vyombo vingine vya habari si chini ya siku 90 kabla ya siku ya uchaguzi.

Pia tangazo hilo litaweka wazi ratiba ya uchaguzi na shughuli zinazohusika na masharti muhimu ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kanuni hizo.

Miongoni mwa mambo ambayo yamepokelewa vyema na vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla, uchaguzi huo utafanyika bila kuwepo kwa mgombea anayepita bila kupingwa kama ilivyokuwa katika chaguzi nyingine za nyuma.

======

UPDATES:

=====​

TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2024​


Limetolewa chini ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2024 (Matangazo ya Serikali
Na. 571, 572, 573 na 574 ya mwaka 2024)

1.0 UTANGULIZI

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 145 na 146 inaelezea uwepo wa Serikali za Mitaa pamoja na madhumuni yake. Mojawapo ya madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Aidha, Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, zinaelekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Lengo ni kuzifanya Serikali za Mitaa ziongozwe kidemokrasia.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 201A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 87A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya kutunga Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo hutumika kuongoza uchaguzi huo. Viongozi wanaochaguliwa katika ngazi hizi ni wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji

Uchaguzi wa mwisho wa Serikali za Mitaa ulifanyika mwezi Novemba mwaka 2019, hivyo, uchaguzi mwingine unatakiwa kufanyika Novemba, 2024. Uchaguzi huu unaongozwa na Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji, Vitongoji na mitaa katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, Matangazo ya Serikali Na. 571, 572 573 na 574 ya Mwaka 2024. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, ninapaswa kutoa Tangazo la Uchaguzi likiainisha ratiba, shughuli za uchaguzi zinazohusika na masharti muhimu ya uchaguzi.

2.0 MASHARTI MUHIMU YA UCHAGUZI​

Masharti muhimu ya kuzingatia katika Uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-

Nafasi zitakazogombewa:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu ni:-

Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024),

Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo. Kwa nafasi hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024)

Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na

Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024).

Majina na mipaka ya Vijiji na Vitongoji:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, ili kuwafahamisha wananchi majina ya maeneo na mipaka ambayo itahusika katika kujiandikisha na upigaji wa kura, wasimamizi wa uchaguzi watatangaza majina na mipaka ya vitongoji vilivyoko katika eneo la Halmashauri husika siku sabini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji,

mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa mtaa, wajumbe wa Serikali ya Kijiji na wajumbe wa Kamati ya Mtaa.

Maelekezo Kuhusu Uchaguzi:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi wa uchaguzi atatoa maelekezo ya

Uchaguzi siku sitini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi.​


Uteuzi wa Waandikishaji na Waandaaji wa Orodha ya Wapiga Kura:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa watumishi wa umma watakaoandikisha na kuandaa Orodha ya Wapiga Kura siku hamsini na mbili kabla ya siku ya Uchaguzi.

Uandikishaji wa Wapiga Kura:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, uandikishaji na uandaaji wa Orodha ya wapiga kura utaanza siku ya arobaini na saba kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa muda wa siku kumi kwa kutumia fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi katika majengo ya umma na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishaji utafanyika kwenye sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.

Vituo vya Kujiandikisha, Kupiga Kura na Kupigia Kura:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura, kwa maeneo yaliyo chini ya Halmashauri za Wilaya na Mamlaka za Miji Midogo vitakuwa katika ngazi ya kitongoji. Kwa upande wa Mamlaka za Miji (Miji, Manispaa na Majiji), vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura vitakuwa katika ngazi ya mtaa.

Muda wa Kuchukua na Kurudisha Fomu za Uteuzi:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi za uongozi, atatakiwa kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi husika siku zisizopungua ishirini na sita kabla ya siku ya uchaguzi kwa kadri itakavyoelekezwa na Msimamizi wa Uchaguzi na kutakiwa kurejesha fomu husika ndani ya muda wa siku saba tangu siku ya kwanza ya uchukuaji wa fomu iliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi.

Wagombea wa nafasi za uongozi:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi watatakiwa kuwa wanachama na wadhamininiwa wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu.

Utaratibu wa uteuzi wa wagombea:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi husika siku kumi na tisa kabla ya tarehe ya Uchaguzi kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

Utaratibu wa uteuzi wa mgombea pekee:​

Endapo kutakuwa na mgombea mmoja halali wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji, kitongoji, ujumbe wa Halmashauri ya kijiji, uenyekiti wa mtaa au ujumbe wa kamati ya mtaa Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi atamteua mwombaji huyo kuwa mgombea pekee kwa nafasi aliyoomba.

Pingamizi kuhusu uteuzi:​

Mgombea au mtu aliyeomba kuteuliwa anaweza kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea. Pingamizi dhidi ya uteuzi wa wagombea litawasilishwa kwa maandishi kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika muda wa siku mbili tangu uamuzi au uteuzi ulipofanyika na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atasikiliza na kutoa uamuzi katika muda usiozidi siku mbili kuanzia siku ya kupokea pingamizi hilo.

Kamati ya Rufani:​

Kutakuwa na Kamati ya Rufani katika kila Wilaya ambayo itasikiliza pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea katika Wilaya husika. Wajumbe wa Kamati ya Rufani watateuliwa siku saba kabla ya siku ya uteuzi wa wagombea.

Ukomo wa kuwa Madarakani:​

Nafasi zote zinazogombewa zilikuwa na uongozi kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, viongozi hao watakoma kushika nafasi za uongozi siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea uongozi chini ya Kanuni hizi.

Upigaji wa Kura:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, kura zitapigwa katika namna itakayozingatia usiri na kwa kutumia karatasi maalum za kupigia kura ambazo zitatakiwa kutumbukizwa katika masanduku maalum ya kupigia kura.

Waangalizi wa ndani wa uchaguzi:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi wataruhusiwa kuangalia uchaguzi baada ya kupata kibali cha Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa. Maombi ya kibali cha uangalizi wa uchaguzi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa ndani ya muda wa siku ishirini na moja baada ya Tangazo la Uchaguzi kutolewa.

Elimu ya Mpiga Kura:​

kwa mujibu wa Kanuni hizi, taasisi yoyote inayotaka kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi, itatakiwa kuwasilisha maombi ya kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kwa Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya Mpiga kura ulioandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kampeni za Uchaguzi:​

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, kampeni za uchaguzi zitafanyika siku saba kabla ya siku ya uchaguzi. Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.

Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3) (Matangazo ya Serikali Na. 571, 572, 573 na 574) ya mwaka 2024, ninautangazia umma wa Watanzania na vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara. Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.

Ninawatakia uchaguzi mwema, amani na utulivu katika kipindi chote cha uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni, upigaji kura, wakati wa kutangaza na kupokea matokeo ya uchaguzi.​


3.0 RATIBA YA UCHAGUZI
Ratiba ya Uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo:-

NA.
TUKIO
TAREHEMHUSIKA
1.Tangazo la Uchaguzi kwa Umma15 Agosti, 2024Waziri
2.Utoaji Elimu ya Mpiga Kura16 Agosti, 2024Katibu Mkuu
3.Maombi ya kuangalia uchaguzi30 Agosti -17
Septemba, 2024
Katibu Mkuu
4.Tangazo la majina na mipaka ya Vijiji, Vitongoji na mitaa16 Septemba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
5.Uteuzi wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Vituo.19-25 Septemba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
6.Maelezo kuhusu Uchaguzi26 Septemba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
7.Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi na wasimamizi wa vituo30 Septemba,2024Msimamizi wa Uchaguzi
8.Uteuzi wa waandikishaji wa wapiga kura.6 Oktoba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi Uchaguzi
9.Viapo kwa waandikishaji wa wapiga kura, wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi6 - 8 Oktoba, 2024Msimamizi wa uchaguzi
10.Elimu kwa waandikishaji wa wapiga kura6-8 Oktoba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
11.Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura11-20 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
12.Kubandikwa kwa Orodha ya Wapiga Kura21 Oktoba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
13.Ukaguzi wa Orodha ya Wapiga Kura21-27 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
14.Pingamizi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura21-27 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
15.Uamuzi kuhusu pingamizi27-28 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
16.Marekebisho ya Orodha ya Wapiga Kura27-28 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi Msaidizi
17.Kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi28-29 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
18.Uamuzi wa rufaa28-31 Oktoba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
19.Kukoma uongozi kwa viongozi waliopo madarakani25 Oktoba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
20.Kuchukua fomu za kugombea01 Novemba, 2024Msimamizi Msaidizi wa
21Kurejesha fomu za kugombea01-07 Novemba,
2024
Msimamizi Msaidizi wa
22.Uteuzi wa Kamati ya Rufani01 Novemba, 2024Katibu Tawala wa
23.Semina kwa Kamati ya Rufani04 Novemba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
24.Uteuzi wa wagombea8 Novemba, 2024Msimamizi Msaidizi wa
25.Uwasilishaji wa pingamizi kuhusu uteuzi8-9 Novemba,
2024
Mwombaji/M gombea
26.Uamuzi wa pingamizi kuhusu uteuzi8-10 Novemba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
27.Kukata rufaa dhidi ya uamuzi kuhusu pingamizi la uteuzi10-13 Novemba,
2024
Mwombaji/M gombea/Msi
28.Uamuzi wa kamati ya rufaa10 - 13 Novemba,
2024
Kamati ya Rufani
29.Uwasilishaji wa ratiba za mikutano ya kampeni
kutoka katika Vyama vya Siasa
14 Novemba, 2024Vyama vya Siasa/ Msimamizi
30.Uwasilishaji wa ratiba za mikutano ya kampeni kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya17 Novemba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi
31.Kuanza kwa kampeni20 - 26 Novemba,
2024
Msimamizi wa Uchaguzi
32.Siku ya Uchaguzi27 Novemba, 2024Msimamizi wa Uchaguzi

Kwa Tangazo hili, Wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura, kugombea na kushiriki katika Uchaguzi huu ili kupata viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mohamed O. Mchengerwa (MB.)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA)

15 Agosti, 2024
 

Attachments

..uchaguzi serikali za mitaa utasimamiwa na Mh.Mchengerwa Waziri wa Tamisemi.

..Mh.Mchengerwa na mkwe wa Rais Samia ambaye chama chake kinashiriki.
Unamaanisha nini?
Unataka kusema kwamba huyo Waziri Mchengerwa siku za kupiga kura atakuwepo kwenye vituo vyote kabisa vya kupigia Kura hapa Tanzania ili aweze kupiga Kura za kuwapatia ushindi wagombea wa Uchaguzi wanaoungwa mkono na mama mkwe wake au????

Nafikiri hoja ya msingi kabisa hapa ni kupigana "kufa na kupona" ili tupate Katiba Mpya ya nchi ambayo ni nzuri itakayoweza kutupatia Serikali ya Kidemokrasia inayowajibika kwa Wananchi. Hii itasaidia kuleta hali ya kuaminiana miongoni mwa Raia.
 
Unamaanisha nini?
Unataka kusema kwamba huyo Waziri Mchengerwa siku za kupiga kura atakuwepo kwenye vituo vyote kabisa vya kupigia Kura hapa Tanzania ili aweze kupiga Kura za kuwapatia ushindi wagombea wa Uchaguzi wanaoungwa mkono na mama mkwe wake au????
Kwani wewe ulivyosoma civics topic ya demokrasia hukuelewa tawala?
 
Unamaanisha nini?
Unataka kusema kwamba huyo Waziri Mchengerwa siku za kupiga kura atakuwepo kwenye vituo vyote kabisa vya kupigia Kura hapa Tanzania ili aweze kupiga Kura za kuwapatia ushindi wagombea wa Uchaguzi wanaoungwa mkono na mama mkwe wake au????

Nafikiri hoja ya msingi kabisa hapa ni kupigana "kufa na kupona" ili tupate Katiba Mpya ya nchi ambayo ni nzuri itakayoweza kutupatia Serikali ya Kidemokrasia inayowajibika kwa Wananchi. Hii itasaidia kuleta hali ya kuaminiana miongoni mwa Raia.
Hapo kwenye paragraph ya mwisho umemaliza kila kitu. Kudos
 
Unamaanisha nini?
Unataka kusema kwamba huyo Waziri Mchengerwa siku za kupiga kura atakuwepo kwenye vituo vyote kabisa vya kupigia Kura hapa Tanzania ili aweze kupiga Kura za kuwapatia ushindi wagombea wa Uchaguzi wanaoungwa mkono na mama mkwe wake au????

Nafikiri hoja ya msingi kabisa hapa ni kupigana "kufa na kupona" ili tupate Katiba Mpya ya nchi ambayo ni nzuri itakayoweza kutupatia Serikali ya Kidemokrasia inayowajibika kwa Wananchi. Hii itasaidia kuleta hali ya kuaminiana miongoni mwa Raia.

..hujuma haipo ktk kudumbukiza kura tu.

..inaanzia kwenye kanuni za uchaguzi, kuandikisha wapigakura, kuandikisha wagombea na mawakala, kuandikisha wasimamizi, kupiga na kuhesabu Kira, kutangaza washindi.

..mratibu na msimamizi wa shughuli zote hizo nyeti ni, Mh.Mchengerwa mkwe wa Rais Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo kinachoshiriki uchaguzi.
 
..hujuma haipo ktk kudumbukiza kura tu.

..inaanzia kwenye kanuni za uchaguzi, kuandikisha wapigakura, kuandikisha wagombea na mawakala, kuandikisha wasimamizi, kupiga na kuhesabu Kira, kutangaza washindi.

..mratibu na msimamizi wa shughuli zote hizo nyeti ni, Mh.Mchengerwa mkwe wa Rais Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo kinachoshiriki uchaguzi.
Je, unaelewa maana ya "Serikali ya kidemokrasia na inayowajibika kwa Wananchi???"
Je, unaelewa maana ya Utawala wa Sheria??
FYI: Vitu hivyo vikiwepo hizo hujuma unazodai kuwepo basi hazitapata nafasi kufanyika.

Tatizo tulilonalo hapa Tanzania ni kwamba:-
1. Katiba iliyopo siyo nzuri hata kidogo, ni Katiba mbovu.
2. Hakuna Serikali Wala Utawala wa kidemokrasia unaozingatia Rule of law.
3. Serikali haiwajibiki kwa Wananchi.

Vyote vitatu kwa pamoja ndio kiini Cha kuwepo kwa matatizo mengi au yote ya Kiutawala yaliyopo hivi Sasa hapa nchini, pia imesababisha hali ya Wananchi kukosa kuaminiana.
 
Je, unaelewa maana ya "Serikali ya kidemokrasia na inayowajibika kwa Wananchi???"
Je, unaelewa maana ya Utawala wa Sheria??

..Ccm hawaangalii katiba na sheria, wanafuata utashi wa Raisi /Mwenyekiti wao.

..Na ameteua Mh.Mchengerwa, mkwe wake, kuratibu na kusimamia uchaguzi.

..Kuna Watanzania milioni 60+, kweli Raisi ameshindwa kupata Mtanzania mwenye sifa kusimamia uchaguzi serikali za mitaa, mpaka ateue mkwewe?
 
..uchaguzi serikali za mitaa utasimamiwa na Mh.Mchengerwa Waziri wa Tamisemi.

..Mh.Mchengerwa ni mkwe wa Rais Samia ambaye chama chake kinashiriki.
Bongo maigizo, mtu na mkwewe, halafu kuna watu wanategemea kushinda, Waziri wa mapolisi nae wa visiwani, lazima mkae tu.

Bada nasimama na Nape, kauli yake ilikuwa ya kishujaa, lakini wengine hamkuelewa,
 
Bongo maigizo, mtu na mkwewe, halafu kuna watu wanategemea kushinda, Waziri wa mapolisi nae wa visiwani, lazima mkae tu.

Bada nasimama na Nape, kauli yake ilikuwa ya kishujaa, lakini wengine hamkuelewa,
CCM kuendelea kubaki madarakani au kushinda Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa
 
Back
Top Bottom