KERO TAMISEMI kuwanyima watumishi wa umma stahiki zao kwa sababu ya mfumo ambao hata hamjazingatia mazingira yao ya kazi ni ukatili mkubwa kwao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

kichongeochuma

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2024
Posts
1,669
Reaction score
2,864
TAMISEMI inacheza na maisha ya watumishi wa umma , kwamba hawato pata stahiki zao za kupanda madaraja kwa kisingizio cha PEPMIS mfumo ambao unahitaji mda kuuelewa na unahitaji vitendea kazi ni kuwafanyia ukatili mkubwa watumishi

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba mfumo huu kwenye simu na vishkambi unasumbua angalau utumie computer halafu , kifupi ni mfumo ambao haujazingatia kabisa hali halisi na mazingira ya watumishi wa umma ndani ya nchi hii.

Lakini cha ajabu watumishi wana ambiwa hawata panda kisa huo mfumo!? Huu utakuwa ni unyanyasaji mkubwa kwa watumishi wa umma ambao wamewajibika kwa miaka mitatu au zaidi halafu jambo la miezi miwili tuu tena ambalo mmelianzisha kwa pupa bila kuzingatia mazingira wa watumiaji likawe kikwazo cha kuwakosesha haki zao huo ni UKATILI mkubwa sana kwa watumishi.

Pia soma: Serikali kutolipa mishahara watumishi kwa kisingizio cha kutojaza majukumu yao kwenye mfumo wa ESS ni unyang'anyi usiotumia Silaha
 
Mimi natamani tu kujua hizo hela za mishahara ya hao watumishi wanazowasitishia kwa kushindwa kujaza taarifa kwenye huu mfumo wao mpya, huwa wanazipeleka wapi!! Maana wahuni siyo watu wazuri hata kidogo.
 
TAMISEMI inacheza na maisha ya watumishi wa umma , kwamba hawato pata stahiki zao za kupanda madaraja kwa kisingizio cha PEPMIS mfumo ambao unahitaji mda kuuelewa na unahitaji vitendea kazi ni kuwafanyia ukatili mkubwa watumishi...
ess.utumishi.go.tz
kichongeochuma ulichokiandika ni sahihi 100% lakini mimi nikukosoe pakubwa kwa kupeleka hizi lawama Wizara ya TAMISEMI chini ya Mchengerwa. Lawama zako inabidi uzipeleke Utumishi (yaani Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) chini ya Waziri George Simbachawene na ndiyo maana huo mfumo unagusa watumishi wote wa mashirika yote ya umma, idara, wakala, wizara zote na hiyo TAMISEMI ikiwemo badala ya wale tu walioko chini ya TAMISEMI. Ambao hawaguswi na huo mfumo wa Utumishi wako na leseni ya kuendesha gari maalum kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na abiria walio ndani ya gari. Sina hakika kama umeelewa hii
 
Inaumiza sana!

Unampigia IT anasema mtandao unasumbua halafu anakuambia uwe unajaribu jaribu labda subtasks utaziona kwenye dashboard ya implementation and monitoring ambayo tasks hazionekani Ili uandike progress na asilimia!!

Kuna tatizo la nchi yetu kufanya maamuzi kutokana na "knee jerk reactios"

Nadhani wanataka kufanya divide and rule kwenye hii ishu,wachache wapande wengine wasipande na kusababisha confusion!!

Huyo simbachawene hajawahi kuwa mtumishi wa umma hawezi elewa how it means kuwa mtumishi wa umma!

Pale unapompa konda ubunge na kuwa kwenye wizara ya watumishi wa umma!

Sad really sad!
 
Watumishi wengi waliochini ya TAMISEMI hawapendi kusumbuka. Wanapenda maisha yale yale yasio na changamoto au jambo jipya. Hata hizi Opras zilikaa miaka na miaka bado kuna waliokuwa hawataki kujaza.

Lazima tukubali mabadiliko. Penati ya kukosa mishahara labda itasaidia. Pengine pangeongezwa muda lakini Kwa hali ilivyo hata iongezwe miaka mitano bado kuna watu watabweteka na wakati wa kupewa penati watalalamika
 
Watumishi wa nchi hii ni wanyonge mpk mnatoa huruma. Kila uonevu mnafanyiwa na serikali ya ccm lkn hamna kitu mnafanya.

Ndiyo maana May mosi mkaletewa wadudu wakatrend mpk sikukuu yenu ikafunikwa.
 
𝔸𝕔𝕙𝕒 π•œπ•¦π•€π•šπ•œπ•šπ•π•šπ•«π•’ π•žπ•’π•Ÿπ•–π•Ÿπ•  π•ͺ𝕒 π•žπ•šπ•₯π•’π•’π•Ÿπ•š 𝕨𝕖𝕨𝕖,π•¦π•Ÿπ•’ 𝕣𝕖𝕛𝕖𝕒 π•ͺ𝕠π•ͺ𝕠π•₯𝕖 π•šπ•Ÿπ•’π•ͺπ• π•€π•–π•žπ•’ π•œπ•¦π•¨π•’ π•žπ•₯π•¦π•žπ•šπ•€π•™π•š 𝕙𝕒π•₯𝕒 π•‘π•’π•Ÿπ••π•’ 𝕕𝕒𝕣𝕒𝕛𝕒 π•œπ•šπ•€π•’ π•‘π•–π•‘π•žπ•šπ•€?

π•Šπ•–π•£π•šπ•œπ•’π•π•š π•ͺ𝕒 π•žπ•’π•žπ•’ π•€π•šπ•  π•œπ•’π•₯π•šπ•π•š π•œπ•’π•žπ•’ π•¦π•Ÿπ•’π•§π•ͺπ• π••π•™π•’π•Ÿπ•š,π•žπ•’π•žπ•’ π•ͺπ•¦π•œπ•  π•œπ•’π•«π•šπ•Ÿπ•š,π•‘π•¦π•Ÿπ•˜π•¦π•«π•’ π•žπ•’π•£π•¦π•¨π•–π•£π•¦π•¨π•–
 
Kwanini kwenye waraka wa kupanda madaraja wakaweka 60% kama sifa ya kupanda daraja ???,
𝔸𝕔𝕙𝕒 𝕑𝕒𝕑𝕒𝕣𝕒 𝕨𝕖𝕨𝕖,π•™π•¦π•›π•¦π•š π•œπ•¦π•€π• π•žπ•’ π•Ÿπ•’ π•œπ•¦π•–π•π•–π•¨π•’,𝕙𝕖𝕓𝕦 π•€π• π•žπ•’ 𝕦𝕖𝕝𝕖𝕨𝕖 π•Ÿπ••π•  𝕦𝕝𝕖π•₯𝕖 π•π•’π•¨π•’π•žπ•’ π•«π•’π•œπ• 
 
Hapana watu hawana tatizo na pepmis bali tatizo ni pepmiss ilivyo anzishwa na jinsi isivyo sadifu uhalisia wa mazingira. Ya watumishi wenyewe
 
Simba Chawene sidhan kama anajua kuwa kuna watumishi wanatumia siku mbili kufika kwenye vituo vyao vya kazi
 
Mf
Mfumo unahitaji bundle lkn fedha ya bundle hawatoi. Maeneo mengine ili mtu apate mtandao ni mpaka afunge safari ya 30km kwa kutumia gharama zake halafu hata elimu tu ya namna gani wana utumia huo mfumo wamepewa wakuu wa idara pekee,watumishi wa ngazi za chini hakuna.

Sasa juzi kuna dogo ni jirani yetu ni MWL kaja likizo.
Kanifuata akihitaji nimsaidie kama nina uzoefu na hayo mambo,kuanza kumuelekeza kuangalia tayari katuma taarifa zake ila bado hazijapitishwa na msimamizi wake ambaye ni Mkuu wa shule.


Nikamuambia kuwa wewe wajibu umeshafanya,bado mkuu wako ndiye anapaswa kupitisha. Maajabu akaniambia kuwa Mkuu wake hajui hata hatua moja kwenye huo mfumo na kwamba na hataki kumpatia Mwl mwingine kufanya majukumu hayo kwa niaba yake kama walivyoelekezwa kwamba kama kuna ambaye ana uzoefu kidogo basi apewe nywila ili atekeleze wajibu huo.

Lkn pia naona ya kwamba unyanyasaji hautaishia kukosa sitahiki zao tu bali pia hata kunyanyasika KINGONO. Tuseme jamaa akikabidhiwa kushika usukani kwenye hicho kitengo halafu kuna madame aliwahi kupewa fomu za maombi ya kutoa uchumi wa kati akagoma,unadhani hapa hatogomewa na yeye kupitishiwa kazi zake mpaka aridhie na yeye kupokea maombi ya mdau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…