Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Madeni ya jumla ya Sh21.7 bilioni ya wazabuni wa vyakula katika shule za msingi na sekondari kwa mwaka 2023/24 yamewasilishwa hazina kwa ajili kuhakikiwa na kulipwa.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 29, 2024 na Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Bernadeta Mushashu.
Mbunge huyo amehoji ni lini Serikali italipa madeni ya wazabuni wanaotoa huduma za vyakula kwenye shule mbalimbali tangu mwaka 2023 hadi 2024.
Akijibu swali hilo, Katimba amesema Serikali imekuwa ikipokea madeni mbalimbali ya wazabuni wa chakula kwa shule za msingi na sekondari za Serikali kutoka katika halmashauri zote.
“Madeni hayo yamekuwa yakilipwa baada ya uhakiki na kadiri ya upatikanaji wa fedha. Mwaka 2020/21 – 2022/23 Serikali imelipa wazabuni wa chakula shuleni kiasi cha Sh26.3 bilioni,” amesema.
Amesema mwaka 2023/24 Ofisi ya Rais –Tamisemi imekusanya madeni ya wazabuni wa chakula katika shule za msingi na sekondari yenye jumla ya Sh21.7 bilioni (shule za msingi Sh761.8 milioni na Sekondari Sh20.9 bilioni).
BUNGENI