TAMISEMI michezo sio chombo cha propaganda, tafuteni njia nyingine ya kupenyeza siasa zenu

TAMISEMI michezo sio chombo cha propaganda, tafuteni njia nyingine ya kupenyeza siasa zenu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kama mdau wa michezo, nina wasiwasi mkubwa kuona jinsi siasa inavyozidi kuingia kwenye michezo, hasa kwenye mpira wa miguu ambao unaunganisha Watanzania wengi. Michezo inapaswa kuwa eneo la umoja, burudani na uwanja wa haki kwa wote, bila kuingiliwa na masuala ya kisiasa. Kitendo cha kutumia mechi kama jukwaa la kuhamasisha ajenda za kisiasa ni kuvunja kanuni za FIFA na kuhatarisha utulivu wa michezo wenyewe.
5868236704861766938.jpg
TAMISEMI wampaswa kutafuta njia nyingine za kuhamasisha wananchi kuhusu uchaguzi na si kupita na upepo wa michezo. Kukosa ubunifu au kutotumia njia rasmi kama Redio, TV na zingine, za kuhamasisha uchaguzi hakupaswi kuwa sababu ya kuharibu soka nchini, mchezo ambao unakua kwa kasi na unaunganisha watu kutoka kila pembe ya taifa. Michezo haipaswi kuwa chombo cha propaganda; ni sehemu ya kuunganisha watu, sio kuwatenganisha au kuwashawishi katika mwelekeo fulani wa kisiasa.

Soma, Pia: Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii

Tunapaswa kuheshimu michezo na kuiacha iendelee kuwakutanisha wananchi kama sehemu ya furaha, mshikamano na uungwana. Tukiendelea kuingiza siasa katika michezo, tunahatarisha kusababisha migogoro na kuwagawa mashabiki. Kwa kuzingatia kwamba FIFA imeweka wazi kuhusu kutotumia michezo kwa masuala ya kisiasa, ni bora tuzingatie na kujiepusha na utata huu. Michezo inastahili kuendelea kuwa safi, huru na mbali na ajenda za kisiasa.
 
Back
Top Bottom