TAMISEMI, mmebariki Halmashauri kuwa wazabuni wa taasisi zake?

TAMISEMI, mmebariki Halmashauri kuwa wazabuni wa taasisi zake?

Nazi embe

Senior Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
105
Reaction score
123
Niende moja kwa moja kwenye hoja kwa mda sasa serikali imekuwa ikipeleka pesa za maendeleo ya miundombinu katika halmashauri zake mfano pesa za ujenzi wa vituo vya afya, pesa za ujenzi wa madarasa, pesa za ujenzi wa nyumba za watumishi,na pesa hizi zimekuwa zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti ya taasisi husika ambazo zinasimamiwa na halmashauri au zikiingia halmashauri na badae kupelekwa katika taasisi husika.

Sasa kwakua bunge linaendelea tunaomba waziri mwenye dhamana atuambie ikiwa fedha za maendeleo zinatumwa katika halmashauri kulingana na makadilio ya ujenzi wataalam mnaita BOQ inakuwaje halmashauri zimeanza jigeuza wazabuni wa usambazaji wa vifaa vya ujenzi katika miradi hii na ikiwa halmashauri ndio inatoa wataalamu kukagua ubora wa vifaa hivyo iweje leo ndio awe msambazaji sawa tunajua wanaitaji mapato sasa ikiwa wao ndio Serikali tunaitaji wasaidie wafanya biashara kufanya biashara na kukusanya Kodi katika halmashauri zao leo hii na wao wanekuwa wafanya biashara je Kodi wanalipa na je katika sheria za manunuzi wanashuindanishwa na nani kujua ubora wa bidhaa zao ikiwa wao ndio wakaguzi na wao ndio wauzaji.

Tunashuhudia kazi zikifanywa tukiuliza nani anasambaza saruji unambiwa halmashauri, ukiuliza kokoto nk unambiwa halmashauri, ukiuliza mafundi unasikia halmashauri, Kila kitu unasikia halmashauri swali hii kitu kisheria ni sawa kama ni sawa hakuna tatizo kama si sawa hawa watu wa halmashauri wanatoa wapi mamlaka ya kujiamulia mambo yaliyo nje ya utaratibu, au ndio shamba la bibi maana hatuelewi.
 
Genge la majambazi hilo bashungwa Takukururu kamata majizi hayo.
 
Ni utaratibu wa kawaida na unafahamika Kisheria..hiyo ndiyo inaitwa 'force Account' Halmashauri au Taasisi yeyote ya Serikali inanunua vifaa vyote yenyewe na mara nyingi moja kwa moja viwandani kwa bidhaa kama vile mabati nk halafu anatafutwa mzabuni/fundi kwa ajili ya kujenga tu.

Kwenye hili kunakuwepo na Kamati ndogo ndogo za usimamizi zinazoundwa na watu/ wananchi mradi ulipo ambazo husimamia Mapokezi na ugawaji wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi husika.

Utaratibu huu unaaminika kupunguza gharama za ujenzi na umetumika kwenye miradi ya ujenzi wa majengo ya madarasa na vituo vya Afya vilivyojengwa kwa Fedha za mkopo nafuu za IMF.
 
Boss hizo kamati hazipo futilia michezo inavyoenda
 
Back
Top Bottom