TAMISEMI mnapaswa kujiongeza

brokenagges

Member
Joined
Sep 29, 2022
Posts
58
Reaction score
33
Nikiwa natembea mitaa ya mji leo siku ya sikukuu nikawa nimejionea ni jinsi gani serikali imegharamia kutengeneza miundombinu na mazingira ktk miji yetu ili iwe safi na salama kwa wakaaji

Lakini juhudi hizo za serikali zinaishia kudumu kwa muda mfupi sana kwani utunzaji wa hiyo miundombinu umekuwa ni ziro wakurugenzi na viongozi kutoka katika halmashauri za miji/ manispaa ama majiji wao hawahangaiki kabisa ktk kubuni namna bora ya kutunza na kulinda miundo mbinu ama mazingira hayo kwa ujumla wake ili fedha ambayo serikali imegharamia iwe na tija kwa muda mrefu.

Kwanza tuone hili ninalolisema hapa, kwenye hii miji wameajiriwa watu wanaofanya usafi katika haya mazingira je ni kwa nini pia wasipewe kazi ya kuzitolea taarifa za uharibifu sehemu wanazofanya usafi?

Ili mamlaka zifanye bidii ya kukarabati mapema gharama zikiwa ndogo badala ya kusubiri hadi zibomoke kabisa na kuja kufanya matengenezo makubwa na ambayo ni gharama na mzigo kwa serikali na wananchi?

 
Ni wapi hapo Mkuu, tueleze na eneo tuchukue hatua mapema.
 
Mbona unapiga picha kwa hofu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…