ligendayika
JF-Expert Member
- Aug 31, 2012
- 1,183
- 198
Nimekuwa nikisikia kila mara madiwani wa halmashauri fulani wamemwazimia mtumishi fulani tena maeneo mengine madiwani wamemkataa mtumishi fulani labda mkurugenzi au yeyote. Najiuliza kama hivyo hawa madiwani sasa si watakuwa wanafanya wanavyotaka kama mtumishi mekwazana na diwani huko mitaani anakujengea hoja kwa madiwani kadhaa unaazimiwa. Naomba wana JF wenye uelewa tuambieni hii ipo kisheria kama sheria ndo hivyo basi ukiwa mtendaji ambae hutaki kuburuzwa na hawa madiwani unaazimiwa. Nijuzeni