Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Waziri Mchengerwa ametoa taarifa ya uandikishaji ambapo taarifa hiyo imetolewa kimkoa kwa ujumla pamoja na asilimia walizofikisha.
Kama mmepata taarifa za kila mkoa, ina maana taarifa kwenye ngazi ya kata na mitaa pia taarifa hizo zipo, kwanini tunapewa kwa ujumla na si kwa kata na mitaa?
Wanananchi tunastahili taarifa hizi, tupewe. Haya ndio yanasababisha mtu akitafuta taarifa hizi hapati lakini pia ni rahisi taarifa hizi kupikwa, ndio maana mnawafanya CHADEMA waanze kujiwahi kutoa taarifa walizokusanya sababu wanajua huku ndiko mnakoelea, hatua taarifa za kata na mitaa, tutajuaje kama takwimu za mkoa tulizopewa ni sawa?
OR TAMISEMI taarifa hizi zinatakiwa kupatikana katika tovuti kwaajili ya kila mwananchi kuweza kuzipata, na mfanye hivyo.