TAMISEMI tunaomba majumuisho ya mapato ya kila halmashauri kwa mwaka 2018/2019 kwenye tovuti yenu

TAMISEMI tunaomba majumuisho ya mapato ya kila halmashauri kwa mwaka 2018/2019 kwenye tovuti yenu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hadi sasa Tumeingia robo ya pili kwa mwaka 2019/20 lakini tovuti yenu haina majumuisho ya mapato ya kila halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Waziri wakati anatangaza alisema watu wa mapato wanafanya usuluhishi wa mahesabu ndio wataweka, lakini tovuti haina kitu zaidi ya taarifa za mapato ya robo na nusu mwaka, hakuna update zilizofanyika.

Waziri ameshaanza kutoa taarifa za mapato ya robo mwaka huu mpya wa fedha.

Natoa wito wahusika watuwekee hizo taarifa maana zinatusaidia kufanya ulinganifu na kujua kipato cha wananchi wa maeneo tofauti hivyo kujua aina za biashara na mzunguko wa pesa wa maeneo.
 
Hii itakuwa vyema sana kwakweli, tuombe Mungu wapite hapa walione hili hasa kwa ustawi wa mzunguko wa biashara za ndani.
 
Back
Top Bottom