TAMISEMI wafafanua kinachopelekea wanafunzi Kupangiwa Tahasusi (Combinations) tofauti na machaguo yao

TAMISEMI wafafanua kinachopelekea wanafunzi Kupangiwa Tahasusi (Combinations) tofauti na machaguo yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi na Wazazi wengi kupangiwa Tahasusi (Combinations) ambazo hawajazichagua hata kama wana vigezo vya kusoma tahasusi walizochagua.

Soma:
- KERO - Serikali mliangalie hili, inakuwaje mtu anachaguliwa kozi ambayo hajaomba?

- Serikali kuweni makini; inakuaje mtoto ana A ya math, B ya Chemistry, B ya biology na B ya Physics halafu mnampangia combination ya Art?!

Jamii Forums imewasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah kupata ufafanuzi wa malalamiko haya ambaye ameeleza:

Kuna mambo makuu 2 yanayozingatiwa wakati wa kuwapangia wanafunzi tahasusi

Alama anazotakiwa kufikisha mwanafunzi kwenye tahasusi husika (cut-off points
Mfano tahasusi ya PCB ina alama 7 lakini mwanafunzi akapata alama 6. Japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa na alama zinazostahili lakini kila tahasusi ina ukomo wa kupokea wanafunzi kutokana na miundombinu iliyopo, idadi ikitimia waliobaki watapangiwa tahasusi nyingine

TAMISEMI waliulizwa pia inawafikishiaje ujumbe wananchi wanaotoa malalamiko yao kupitia mtandao, ambapo alisema;

Katika watu zaidi ya laki moja waliopangiwa shule malalamiko hayawezi kukosekana. Kati ya malalamiko yanayotolewa baadhi ni kutopangiwa shule wanazozitaka, wengi akilini mwao wana majina ya zile shule Kongwe 89, kila mzazi anatamani mtoto wake apangiwe kwenye hizo shule. Sasa hivi kuna shule 532, kila Wilaya na Mkoa zina shule mpya. Kila shule lazima zipelekewe Wanafunzi.

Tuna kituo cha Huduma kwa Wateja ambacho wote wenye malalamiko wanayawasilisha hapo, pale wanatoa maelezo, na kama muhusika hajaridhika na maelezo hayo atapewa mwongozo wa kufikisha malalamiko yako kwa Katibu Mkuu kwa kuandika barua na kuelezea anachokutana nacho, na ambacho hajaridhika nacho na kile anachoamini anastahili kukipata. Wakiipokea wataichambua wakiona kama ana sifa basi watambadilishia.

PIA SOMA
- TAMISEMI wafafanua utaratibu unaotakiwa kufatwa ikiwa mwanafunzi anataka kubadili tahasusi tofauti na aliyopangiwa
 
Yuko sahihi
Pia Unakuta mtoto mfano kafaulu sana masomo ya sayansi halafu kwenye combination kajaza HGK au HGL ambayo ufauli wake Unakuta uko chini kumtendea Haki wanapeleka masomo aliyofaulu sana ambayo ana uwezo nayo kumhurimia asihe kwenda huko asiko na uwezo akafeli vibaya

Ila akitaka kwenda private pia wakiangalia ufauli wake hata wao Kuna Shule watamgomea watamwambia tutakupokea kwenye haya masomo ya sayansi aliyofanya vizuri
 
Hivi waliopangiwa kusoma A level ila wanataka chuo, utaratibu upi unafanyika?
 
Hivi waliopangiwa kusoma A level ila wanataka chuo, utaratibu upi unafanyika?
Kwa nilivyoelewa hapo jaribu kuandika barua kwa Katibu wa TAMISEMI ili kupata msaada. Au la wasiliana na chuo unachotamani utume maombi huenda ukapewa admision
 
Mtu husoma anachotaka toka moyoni. Siyo kumpangia wewe mwisho wa siku akisoma hiyo arts unamnyima ajira.
 
Back
Top Bottom