TAMISEMI yaomba Bajeti ya Tsh. Trilioni 10.1

TAMISEMI yaomba Bajeti ya Tsh. Trilioni 10.1

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imeliomba Bunge likubali kuidhinisha Sh10.1 trilioni ambazo ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa wizara hiyo.

Fedha hizo ni ongezeko la Sh981 bilioni ikilinganishwa na fedha zilizoombwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, kiasi cha Sh9.1 trilioni.

Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa ametoa maombi hayo bungeni leo Jumanne Aprili 16, 2024 wakati akisoma makadirio ya mapato na mtumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25, yanayohusisha mafungu ya Tamisemi, Tume ya Utumishi wa Walimu na mikoa inayojumuisha halmashauri 184.

Mchengerwa amesema fedha hizo zinahusisha Sh3.4 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya hizo, Sh2.2 trilioni ni fedha za ndani na Sh1.1 trilioni ni fedha za nje.
 
Ni karibu 30% ya bajeti nzima ya serikali, yaweza kuwa tamisemi ni kubwa kuliko tunvyodhani.
 
Back
Top Bottom