Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Kwahiyo wale walioenguliwa kwa kigezo hiki wanakuwa ndio wamerudi kwenye kinyang'anyiro au ndio wameondolewa hivyo hivyo kwa uonevu?
====
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) imesema ujasiriamali ni kazi halali inayotambulika kiserikali, si sawa kutumika kuwaengua wagombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Hayo yamesemwa leo Jumanne, Novemba 12, 2024 na Mwanasheria wa Tamisemi, Mihayo Kadete wakati akijibu maswali kwenye kikao kazi na wahariri kinachofanyika jijini Dar es Salaam.
Kupata nyuzi kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kadete amesema si sahihi mgombea kuenguliwa kwa kigezo tu amejaza kazi halali ni mjasiriamali; na mtu aliyeenguliwa akate rufaa kwa kuwa hiyo ni kazi halali.
Kadete amesema mgombea ambaye hajajiandikisha kupiga kura kwenye eneo lake ni moja ya sababu ya kukosa sifa ya kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27, 2024.
"Mtu akatwe kwa kukosa sifa na si kukatwa kwa kudhamiria bali akatwe kwa haki," amesema Kadete.
Semina hiyo ya siku moja ya masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 imeandaliwa na Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Mwananchi