Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
Habari ya TAMISEMI inasema
"Wakuu wa Wilaya wanajukumu kubwa la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikizingatiwa kuna fedha nyingi zimepelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu, Afya na Miundombinu.
Pia Wakuu wa Wilaya wanapaswa kuwafuata wananchi kusikiliza na kutatua kero zao!Ikumbukwe kuwa Wakuu wa Wilaya zaidi ya 100 hawana Magari yakuwawezesha kutekeleza shughuli zao ipasavyo!Tuwajali Wakuu wetu wa Wilaya, Gari ni kitendea kazi muhimu katika utekelezaji wa majukumu yake."
Magari haya bhana yamekiuwa yakizalishwa Kwa muda mrefu lakini Mwisho wa uzalishaji ni 2013, Ambapo new model yake ndio TOYOTA LANDCRUISER PRADO V8, then LC 300. Hizi gari Wanazosemea wao Bei kulingana ya mwaka 2013.
Fuel: Petrol
Engine Code: 2TR
Seats: 5 with 5 Doors
BEI: 39,000,000 - 42,000,000
Bajeti Iliyowekwa ni BILIONI 119
-Magari 56 ni sawa na 2,240,000,000( BILIONI 2.2). Ukitoa kwenye Bajeti inabaki BILIONI 116.7 ambayo wamesema inaenda kwenye Ukarabati, wa Majengo.
sasa Ukarabati wa BILIONI 116 ni ukarabati wa MJI MZIMA au wanajenga Majengo mapya, mana kuna majengo na Nyumba.
UPDATE
Kama nilivyowaambia ndugu zangu, Hapa tulikuwa tunapewa tu Taarifa, tumepigwa hapa hizi gari zilizonunuliwa ni zaidi ya Milioni 600 Gari moja kweli hizi pesa hazikutosha kuweka Moram barabarani kipindi hiki cha mvua.. alafu mtu mmoja ndo anaenda kutumia gari hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amekabidhi magari matatu mapya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Rombo, Mwanga na Same, yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 600 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo.
Akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za RC wa Kilimanjaro, Babu amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.
RC Babu amesema Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na Wakuu wa Mikoa kukosa magari ambapo Mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya Wakuu wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za Kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama kubwa.
CHANZO: MillardAyo

2012 TOYOTA LAND CRUISER PRADO TX
Engine: 2,690ccFuel: Petrol