LGE2024 TAMISEMI yawanoa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online TV) kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha hawatoi taarifa kwa upendeleo

LGE2024 TAMISEMI yawanoa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online TV) kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha hawatoi taarifa kwa upendeleo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Inashangaza pale unakuta kichwa cha habari kutoka online TV kinakuwa kama kaandika Lucas Mwashambwa, nilikutana nayo juzi wakati nataka nichukue risiti wakawa wamefuta bana. Kwa jinsi ilivyoweka wallah ule mwandiko ulikuwa wa Lucas Mwashambwa.

======

Screenshot_20241113_150955_Instagram.jpg

Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais - TAMISEMI) leo imekutana na waandishi wa Habari za Mitandaoni (Online TV) katika ukumbi wa Ofisi za TARURA Jijini Dar es Salaam wa ajili ya kuwapa mafunzo mbalimbali kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika hivi karibuni.

Kupata habari za kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa:LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Screenshot_20241113_151005_Instagram.jpg

Licha ya kufundishwa kuhusu kanuni za Uchaguzi lakini pia Waandishi wametakiwa kutoa taarifa bila upendeleo wowote kwa chama kimoja bali vyama vyote vipate haki sawa katika kutoa taarifa hizo.

Screenshot_20241113_151025_Instagram.jpg
 
"Wameshatishwa" na mkwe. Kitakachofuatia ni kusifu na kupongeza pasipo kikomo.
 
Back
Top Bottom