25 July 2024
viongozi wa genge la Sinaloa Cartel, Ismael Zambada Garcia (El Mayo) na Joaquin Guzman Lopez watiwa nguvuni baada ya operesheni kabambe
Idara ya Sheria nchini Marekani imetoa taarifa ifuatayo kutoka kwa Mwanasheria Mkuu Merrick B. Garland kuhusu kukamatwa kwa wanaodaiwa kuwa viongozi wa Sinaloa Cartel, Ismael Zambada Garcia (El Mayo) na Joaquin Guzman Lopez:
"Idara ya Sheria imewaweka kizuizini viongozi wawili vigogo wanaodaiwa kuwa wa genge Sinaloa Cartel la nchini Mexico, mojawapo ya magenge yenye ukatili na yenye nguvu zaidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani.
Ismael Zambada Garcia, au "El Mayo," mwanzilishi mwenza wa Cartel, na Joaquin Guzman Lopez, mtoto wa mwanzilishi wake mwingine, walikamatwa leo huko El Paso, Texas.
Wanaume hao wawili wanakabiliwa na mashtaka mengi nchini Marekani kwa kuongoza operesheni za uhalifu za Cartel, ikiwa ni pamoja na mtandao wake hatari wa kutengeneza fentanyl na ulanguzi.
El Mayo na Guzman Lopez wanajiunga na orodha inayokua ya viongozi na washirika wa genge la Sinaloa Cartel ambao Idara ya Sheria inawajibisha nchini Marekani.
Hiyo inajumuisha mwanzilishi mwenza mwingine wa Cartel, Joaquin Guzman Loera, au “El Chapo”; mwana mwingine wa El Chapo na anayedaiwa kuwa kiongozi wa Cartel, Ovidio Guzman Lopez; na anayedaiwa kuwa kiongozi wa Cartel, Néstor Isidro Pérez Salas, au "El Nini."
Fentanyl ndio tishio baya zaidi la dawa za kulevya ambalo nchi yetu Marekani imewahi kukabili, na Idara ya Sheria haitapumzika hadi kila kiongozi wa kikundi, mwanachama, na mshirika anayehusika na kutia sumu hii katika jamii zetu watiwe mbaroni na wawajibike kwa biashara hii haramu.
Source : Attorney General Merrick B. Garland Statement on Arrests of Alleged Leaders of the Sinaloa Cartel Ismael Zambada Garcia (El Mayo) and Joaquin Guzman Lopez
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Marekani, Bw. Merrick B. Garland Atoa Taarifa kuhusu Kukamatwa kwa Viongozi Wanaodaiwa wa Kundi la Sinaloa Bw. Ismael Zambada Garcia (El Mayo) na Bw. Joaquin Guzman Lopez