Ni weekendi iliyopita, watanzania wengi sana walitumiwa jumbe za simu kuwa mgombea mmoja wa chama cha siasa atamwaga damu.
Mimi binafsi nilikuwa suijasikia kauli ya mwanasiasa huyo na hata kama tungesikia sisi siyo mambumbumbu kutochagua nani anatufaa.
Lakini cah kushangaza ni pale mamlaka husika zilipojifanya kutojua kabisa na hata kutofanya uchunguzi kidogo to eti code no +3.... ni yawapi wakati ni Finland. lakini pia walisema kuwa watawauliza makampuni ya simu wakati wakijua kabisa kuwa makampuni hayo hayana code hizo, na kwa ujumbe ule hakuna ambaye angekubali.
Lakiini sasa jana jioni CCM wametuma jumbe zenye kushabihiana na zile japo tofauti ni wamesema tusicahgue wapinzani.
Kwanza wana JF kuna watu wamepata hizi?
Na hatuna sababu ya kuamini kuwa waliotuma ni hao hao CCM kwa kutumia mtandao?? maana mbaya wa CHADEMA kwa sasa ni CCM peke yake na hakuna mwingine!!
Sasa kama umegombana na mtu, halafu ukadhurika, Je mtuhumiwa wa kwanza si mbaya wako!?
1. Kwanza CCM tunawashauri, kama wapiga kura wamechoka basi wasubirini tu maana kama ni amani walinzi ni wananchi na siyo chama ,
2. Chama hiki kinafahamika na mazuri yaliyofanyika yanajulikana, lakini na uchovu wake unaonekana!
3.Chama kiache kabisa kuwapotosha watu kwa hoja zisizokuwa na maana na za uwongo mkubwa.
4. Chama kiombe tu kura kwa watu kistaarabu bila ya kumhofia mtu na kumtafutia hoja ambazo hata yeye mwenyewe hajawahi kuziota.
5. CCM waachie wapiga kura waamue nani wa kuwatumikia siyo lazima wao tu.