Tamko la Umoja wa Kizazi cha Kuhoji(UTG) kuhusu hali ya usalama nchini na kupotea kwa Ben Saanane

Ripoti yenu ni nzuri UTG na inasikitisha kumbe kuna watu wengi hivi wanapotea kwa njia ya kutatanisha.
 
Kwanini UTG wasitafute namna ya kufanya independent DNA tests za mabaki ya miili iliyozikwa kule Bagamoyo badala ya kutegemea Serikali kupitia Mkemia Mkuu? Kamwe hamtapata ushirikiano kutoka vyombo vya Serikali kama mlivyoainisha. Why you keep expecting and insisting on cooperation from the government while you very well know such isn't forthcoming is simply ridiculous.
 
wamefatilia na kuwahoji mwanahalisi waliochapisha habari ben saanane anaonekana kwa marafiki zake
 
Kwani lazima atumie namba mnayojua nyie?Unamlazimisha mtu atumie namba unayojua wewe unamlipia airtime au simu umemnunulia wewe?
Mkuu, hivi huoni kama unajiaibisha kujadili vitu usivyovielewa!
 
Vijana wanafanya kazi nzuri kuliko hata vyama vya siasa!!,
Vyama vya siasa vinalalamika ila havichukui hatua!!
Ila Hawa wameenda extra mile...
Wakiendelea kusimamia wanacho amini wanajenga majina yao vizuri.
 
Naamini humu ndani kuna watu wanafanya kazi makampuni ya simu. Toeni namba ya Ben watusaidie kuangalia mawasiliano yake ya hizo siku mbili
 
Tatizo kubwa watu wengi wanaoajiliwa kwenye vyombo vya usalama ni waliofeli,wameona huko ndipo kunahitaji mazezeta
 
Inasikitisha sana. Ila tumuombe muumba wa mbingu na ardhi atupe wepesi ktk maisha yetu.
Ameen.
 
Kitendo cha serikali kutumia mamilioni ya fedha kupima DNA yafaru John huku ikipuuza kupima DNA kwa miili ya binadamu wenzetu iliyookotwa, hakileti tafsiri nzuri kwa wananchi. Wengi wanaona kuwa serikali inathamini zaidi uhai wa wanyama kuliko watu
Malisa, labda nikushauri. Ukitaka tamko lako liheshimike basi hakikisha lina address core business pekee. This particular phrase and others in the statement sound more political ploys than addressing core business.
 
Vijana wanafanya kazi nzuri kuliko hata vyama vya siasa!!,
Vyama vya siasa vinalalamika ila havichukui hatua!!
Ila Hawa wameenda extra mile...
Wakiendelea kusimamia wanacho amini wanajenga majina yao vizuri.

Ila mkuu, nimeshangazwa na jambo moja tu:-

Kwa nini vyombo vya habari vinavyotumia kodi za wananchi havikuwepo kwenye huu mkutano , pamoja na mada kujulikana mapema kwamba wanaongelea habari za Ben Saanane?

Sijaona, TBC, Uhuru, Mzalendo, Daily News wala Sunday news. Kwa ni ni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…