Tammy Abraham vs Lukaku

Shabani Ajaha

Member
Joined
Aug 18, 2021
Posts
78
Reaction score
60
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea TAMMY ABRAHAM jana alifungia timu yake ya AS ROMA goli pekee lililoipeleka klabu hiyo fainali ya #UECL katika ushindi wa jumla wa magoli 2-1 dhidi ya LEICESTER CITY.
-
ABRAHAM amefunga magoli 25 msimu huu kwenye michuano yote akiwa ndio mchezaji pekee kutoka ENGLAND kufikisha idadi hiyo ya magoli katika Ligi 5 bora Ulaya.
-
Ikumbukwe CHELSEA ilimuuza ABRAHAM kwa pauni milioni 34 na kumnunua ROMELU LUKAKU kwa pauni milioni 97.5.
-
TAKWIMU ZA ABRAHAM NA LUKAKU MSIMU HUU:

ABRAHAM:

[emoji2522] Mechi: 49
[emoji460] Magoli: 25
[emoji2402] Assists: 5

LUKAKU:

[emoji2522] Mechi: 40
[emoji460] Magoli: 12
[emoji2402] Assists: 2

‘Dhahabu ilitupwa JIWE likaokotwa’

#Shabani Ajaha
 
Ligi bora ni england tu hizo ligi zingine ni za mchangani tu
 
unalinganisha magoli 12 ya EPL na magoli 25 ya italy?serious?
 
Tahadhari ni muhimu.

Kilichofanya Chelsea wakamrudisha Lukaku ni performance yake huko Seria A.

Unataka kushawishi wamrudishe T. Abraham kwa sababu ya anavyo perform huko Seria A.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbukeni mchango wa kocha pia kwenye mafanikio ya mchezaji.Tammy Abraham kwa sasa yuko chini ya mtaalam The Special One- Mourinho!! Lazima awe bora kuliko Lukaku aliye chini ya bwana mdogo Tuchel!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…