Tamthilia: JF talk garden, eneo lenye vituko na vitimbi. episode ya 04

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
EPISODE 04

Na mende msafi

Previously in JF talk garden

Nyani Ngabu: (huku akimgeukia mende msafi) hey you dude, hivi unajua bei ya shati uliloligusa. Bei ya hiyo shati ni sawasawa na kontena 9 za makinikia, nauli ya bombadia kutoka dar hadi kwenu mara 14 na inabaki chenchi inayotosha kuwalisha ukoo wenu wote kwa siku 29. Don’t mess with me you basidiyomycota. (kisha anamshika demiss na kuanza kutoka pale katikati ya kundi la watu, watu wanawapisha.)

Nyani ngabu anatoka katikati ya watu kisha anageuka na uliangalia lile kundi

Nyani Ngabu: USA baby…(kisha anatoka nje ya jengo la chit chat akiwa na demiss)

Watu waliobaki wanabaki wanatizamana.

Endelea sasa…..

mende msafi anainua uso wake na kuwaangalia watu waliokuwa katika kile kikundi ambapo walikuwa wakiongelea lile tukio lililotokea muda mfupi uliopita, wengi wao wanamuangalia. Wengine wakionyesha nyuso za masikitiko wengine wakicheka na kutabasamu. mende msafi anatoka pale na kusogea pembeni akiwa na hasira. Anasimama kidogo kisha anamua kupiga hatua kuelekea nje ya jengo la chi chat.

Anafungua ule mlango na kutoka nje. Anaufunga mlango kwa kuubamiza kwa snguvu. Kile kikaratasi kilichoandikwa “general chat, talk about anything that falls under no category on the board, but remember FOLLOW THE RULES” kilichobandikwa kwenye mlango kinadondoka chini. Mende msafi anageuka na kukiangalia huku akiwa katika mstuko. Anakiokota kwa haraka akiwa na wasiwasi. Anakichukua na kujaribu kukirudishia inashindikana kwa sababu gundi yake imeisha nguvu.

Anaangalia kulia na kushoto ili kujua kama kuna mtu anamuangalia, anajiridhisha kuwa hakuna mtu anayemuona. Anaigeuza ile karatasi upande wa nyuma na kutemea mate na kuyasambaza. Kisha anaichukua na kuibandika kisha anasogea mbele kidogo. Anawaza aende sehemu gani ili angalau akatoe stress zake, anaamua kwenda MMU.

Lakini kabla hajafika anasikia mziki nje ya uzio wa JAMIIFORUMS. Unasikika hivi:

tumeipenda wenyewe,(ndi ndiiii)

Chaguo letu wenyewe,(ndi ndiii)

Wavimbe wapasuke,(ndi ndiii)

Watajijua wenyewe,(ndi ndiii)

Acha waisome namba eeeeeeh….

C…..”

Mara mziki unakatishwa na sauti ya mtu inaanza kuongea

Mtu 1: jamani wanakijiji wa kijiji cha makinikia, mwenyekiti wa kijiji anataka kuongea na nyinyi. Tafadhali, popote ulipo acha shughuli zako na tumsikilize mheshimiwa wetu.

Kisha mziki unaruhusiwa tena

“hatunywi sumu hatujinyongiiii…”

Mziki unakatizwa tena. Watu waliokuwa ndani ya majengo tofauti tofauti ndani ya JF wanatoka, eneo la nje linajaa watu wengi..wote wakiwa na shauku ya kutaka kujua ni nini mwenyekiti wao wa kijiji alikuwa anataka kusema.

Mara anaanza kuongea

Mwenyekiti: jamani wananchi wa kijiji changu cha makinikia amani iwe nanyi. Kwanza kabisa nipende kumshukuru mkuu wa mtaa huu wa MAGWANGWALA, ndugu Petro Mapigadebe Madereva kwa uchapakazi wake. Japokuwa kuna watu wanasema eti hafai ila mimi nasema kuwa anafaa na hakuna wa kunipinga maana mimi ndo mwenyekiti. Halafu kuna tabia ya watu kutotaka kufanya kazi wanakaa tu wanapiga soga kama hawa wa kwenye hayo mabanda ya bluu. (watu waliokondani ya eneoo la JF wanaangaliana). Yaani wapo wapo tu. sasa nasema hivi kama wakiendelea hivyo nitalifunga banda hilo na mengine yoote yanayofanana na hili ili watu wafanye kazi”

Mwenyekiti anaongea mambo mengine mengi ambayo yanawafanya watu walioko ndani ya eneo la JF kushikwa na huzuni na hasira na gadhabu pia. Japo wapo wengine wakionyesha kufurahia kauli za mwenyekiti. Malumbano makali yanazuka kati yao.

Mwenyekiti anamaliza kuongea.

Mtu 1: ndugu wanakijiji wa kijiji cha makinikia tunashukuru kwa usikivu wenu

Kisha mziki unawashwa tena…

[“harambeee eee eeee harambe mama harambeeee,(harambee ee harambe mama harambee)x2]

Mwenyekiti, (tumbebee, tumkumbatie tumbusu),

Madereva, (tumbebee, tumkumbatie tumbusu)

Mammvi, (tuliletee, tumchanechane tumtupe)

Likitambi, (tuliwin…….)”

Wimbo unakatizwa kisha kimya, muda ufupi baadaye muungurumo wa gari unasikika kwa muda huku ukipungua taratibu na kisha unapotea kabisa.

Watu wa JF wanaendelea na malumbano kuhusu kauli tata za mwenyekiti wa kijiji chao cha “makinikia”. Wakati wakiendelea kubishana wanaona ule uzio wa waya ukitikisika. Wanageuka kuangalia wanaona sungusungu wa kijiji cha makinikia wakiruka ule uzio na kutua ndani, huku wakiwa na fimbo. wanaJF wanachanganyikiwa. Wale sungusungu wanawasogelea kwa kasi zaidi hali inayowafanya baadhi ya wanaJF kuanza kukimbia kwa kuwaogopa sungusungu. Walinzi wa JF na kwenda kuwawahi wale sungusungu na kujaribu kuongea nao.


Invisible: taratibu wakubwa, taratibu. Ni nini mnakihitaji kutoka kwetu na kwa nini mnakuja kwa shari hivi?

Sungusungu1: (kwa sauti ya ukali) tunamtaka mmiliki wa eneo hili. Bwana maxence mello. Tunamtaka haraka sana.

Je, ni kwa nini sungusungu wanamtaka maxence? Kwa jibu la swali hilo na mengine mengi jiunge nami katika mfululizo wa tamthilia hii.

Kama kuna member yeyote aingizwe katika uhusika wa tamthilia hii fanya hivi, taja ID yake na tabia zake ndani ya JF na utamuona aking’ara kati episode zijazo.

Thank you

Mende msafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…