Tamthilia ya Bibi Titi Mohammed na Prof. Emmanuel Mbogo

Nyumba ya Bibi Titi moja iko Upanga hapa mtaa wa makao makuu ya jeshi, nafikiri ni mtaa wa Magore ule kama nakumbuka vizuri.

Mtaa unaoanzia Palm Beach unaenda kutokea mpaka Diamond Jubilee Hall/Shaaban Robert Secondary na Olympio Primary. My old stomping grounds.

Alikuja kurudishiwa ile nyumba kipindi cha Mwinyi kama sikosei.
 
Kunaweza kukawa na ukweli
Lakini ndio historia haiwez kuwasema wote walioshiriki
Kwa kumsoma muhusika mkuu ndio tutawajua na wengine
Muhusika mkuu ndiyo nani? Maana tunaona kuwa harakati za Uhuru hazikuanzia na Nyerere kama tulivyosadikishwa na kitabu cha historia cha kivukoni.

Allama Mohamed Said anaweka kumbukumbu sawa kuwa harakati zilianza zamani sana.

Unaifahamu historia ya Ikulu ya Dar na kanisa lenye "kibla" la hapo Dar?

Hutopenda kufahamu hayo?
 
Unaonesha jinsi ulivyo ghadhibika. Unaandika maandiko marefu yasiyo na mpango.

Mara vitabu. Mara babu zetu. Mara wazee wetu. Mara Waarabu. Mara Waislam.

Mara "mnataka kuifanya nchi hii ya Kiislam".

Mara hili mara lile. Umeandika mambo kibao lakini hata moja halina maana kwa kuwa unajiandikia tu na wala unachokiandika hukielewi. Ndiyo maana unaambiwa soma rejea uje na hoja.

Lile la "lecturer" wako hata baada ya kuoewa darsa umelirudisha tena kama jina tu bila hoja yoyote.

Hivi nnakuuliza, hujawahi kulazwa hospitali kwa matatizo ya kichwa?

Mara historia nzuri ni kuandikwa na "mtu asiye na upande".

Sasa Tanzania hii ni nani asiye na upande? Wote niwaonao ni wazima kamili na sijaona mtu asiye na upande akitembea. Tumtoe wapi?

Stick kwenye point moja ueleweke. Punguza ghadhab.

Wacha kubabaisha babaisha. Kujifanya unajuwa kumbe huna unalolijuwa.

Kuhusu Waarabu kugaiwa nchi sifahamu fikra hiyo potofu unaitoa wapi? Au unamaanisha WAISLAM?

Maana kama ni Uarabu hata wewe unao. Wewe si mstaarabu?
 
Sasa kati ya maandishi haya uliyoandika na niliyoandika mimi yapi yanaonesha aliyegadhabika!?

Pole sana, sijafundishwa kujibu matusi!
 
Sasa kati ya maandishi haya uliyoandika na niliyoandika mimi yapi yanaonesha aliyegadhabika!?

Pole sana, sijafundishwa kujibu matusi!
Huna hoja tu. Tusi hujatukanwa unavunga umetukanwa, jee ukitukanwa si ndiyo mwao.

Jibu kuhusu "lecturer" wako na AMNUT ulilipata juu huko au hujalipenda au ndiyo akaae kimya kakubali.

Kiislam binti akiletewa pisa huulizwa, fulani kaleta posa umekubali?" Akikaa kimya kakubali.
 
Hizi ni akili mgando hizi! Aliyekwambia kwamba ukianzisha jambo lazima ulimalize wewe ni nani!?

Tangu wakoloni wanaingia Afrika walipokelewa vizuri!? Je, hao waliokuwa wanawapinga wao si wapigania uhuru!?

Mandela ndiye aliyeanziasha harakati za ukombozi S. Afrika? Kwanini anajulikana yeye kwa wengi?

Timu ya mpira inakuwa na wachezaji wengi lakini mwisho wa mchezo anatajwa mchezaji bora mmoja! "Man of the match"

Mtaongea mnayoongea yote lakini kwa Tangayika ' Man of the match" katika harakati za ukombozi atabaki Nyerere leo na hata milele yote

Kuwa "man of the match" hakumaanishi alipigana peke yake, hilo kila mtu analijua! Hao wengine wapo na wataendelea kuenziwa kwa nafasi zao lakini lazima mkubali kuwa hawawezi kuwekwa kwenye "rank" moja na Nyerere! HIKI NDICHO HAMKITAKI LAKINI HAMNA NAMNA LAZIMA MKUBALI TU!

Hata kwenye familia lazima atatokea mmoja atakuwa "juu" na atatambuliwa kama alama ya familia! Hii haimaanishi familia hiyo haina watu wengine!

xxx haya endelea kutukana tena maana ndo kipaji chako xxx
 
AMNUT kutokana na madai yake ya longo longo kama hayo hayo ambayo kila siku mnayataka ya kutaka nchi iwe ya dini ilibidi ijifie natural death tu maana ilikutana na kisiki cha Butiama!

Au kuna jibu zaidi ya hili!
 
AMNUT kutokana na madai yake ya longo longo kama hayo hayo ambayo kila siku mnayataka ya kutaka nchi iwe ya dini ilibidi ijifie natural death tu maana ilikutana na kisiki cha Butiama!

Au kuna jibu zaidi ya hili!
"Madai yake" nani?

Mbona unakuwa muoga muoga wa kuongea?


Ooh funguka tu. Kumbe ulidanganya kuhusu "lecturer"? Yalikuwa ni yako.

Onesha rangi zako kamili wacha kujifungia ndani ya kabati.
 
Wapi wameenziwa na wakati ulikiri juu huko hata majina hujawahi kuyasikia ndiyo kwanza umeanza kuyasikia kutoka kwa Allama Mohamed Said.

Ulikuwa una enzi hewa? Unanchekesha.
 
AMNUT kutokana na madai yake ya longo longo kama hayo hayo ambayo kila siku mnayataka ya kutaka nchi iwe ya dini ilibidi ijifie natural death tu maana ilikutana na kisiki cha Butiama!
viliku
Au kuna jibu zaidi ya hili!

Uncle...
Mimi nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes sikufanya hivyo kwa nia ya
kushusha hadhi ya Mwalimu Nyerere katika harakati za kupigania uhuru
wa Tanganyika.

Nimeandika kitabu hiki kwa nia ya kueleza historia ya TANU na harakati
za kudai uhuru kwa kuwa vitabu vyote vilivyokuwa vimeandikwa vilikuwa
vikianza na Julius Nyerere mwaka wa 1954 TANU ilipoundwa.

Kwa kufanya hivyo historia muhimu ya African Association na TAA hadi
kufika kuundwa kwa TANU ilikuwa imepotezwa.

Nimeanza kuandika nikijua kuwa historia hii haikuwa inatakiwa kwani
kulikuwa na mradi wa TANU yenyewe wa kuandika historia yake ambao
Abdul Sykes alipewa jukumu la kuandika historia hiyo akishirikiana na
Dr. Wilbard Kleruu.

Abdul Sykes hakukamilisha kazi hii alijitoa baada ya kugundua kuwa
historia iliyokuwa inatakiwa kuandikwa si ile anayoijua yeye na Abdul
akijua mengi katika historia ya TANU kwani baba yake alikuwa muasisi
wa African Association mwaka wa 1929.

Sasa unazungumza kuhusu ''ranking,'' sijui utafanya hivyo kwa vigezo
vipi kwani ikiwa ni historia ya TANU hakuna ushahidi mahali popote
unaoonyesha kuwa Nyerere alifika kwa Abdul Sykes 1952 akiwa na
''blue print,'' ya TANU.

Harakati hizi za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika alizikuta
kwa Abdul Sykes na kabla yake yalipita mengi na kulikuwa na wengi
katika juhudi ya kufanikisha lengo hili.

Upo ushahidi wa mchango mkubwa wa Hamza Mwapachu katika kufikia
lengo la kuunda TANU na itoshe tu kuwa mkutano wa kumtia Nyerere
katika uongozi wa TAA uliofanyika nyumbani kwake Nansio, Ukerewe
miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 kati ya yeye Hamza, Abdul Sykes
na Ally Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya.

Hapa sikutaka kukurejesha nyuma 1950 kwenye TAA Political Subcommittee
ambayo wajumbe wake wake walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid
Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven
Mhando
na John Rupia.

Wala sijataka kukuonyesha viongozi wa TAA ambao waliingia katika
uongozina Julius Nyerere pale alipochaguliwa kuwa Rais wa TAA katika
mkutano uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili, 1953.

Viongozi hawa ni: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-
President;

J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri
Dossa Aziz,
Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer na Ally K.
Syke
s - Assistant Treasurer. Committee members Dr. Michael Lugazia,
Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi,
C. Ongalo
na Patrick Aoko.

Sasa huwezi kufanya ''ranking,'' ya mtu mmoja lazima wawe wengi na
unaanza juu hadi unafika chini.

Ukiwa unataka kufanya ''ranking'' inabidi sasa uanze na wajumbe wa TAA
Political Subcommittee uwachanganye na hii Halmashauri ya TAA ya 1953.

Kuna wengine wamehusika sana lakini majina yao huwezi kuyaona hapo
juu mfano Earle Seaton.

Haya ndiyo yaliyonifanya mimi niandike historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika kusahihisha historia iliyokuwapo.

Kuhusu AMNUT nimekwisha eleza hapa kuwa ni jina tu ''Muslim,'' ndilo
linalokufanya wewe ukiite chama cha Waislam.

Waislam chama chao kilikuwa TANU.

AMNUT iliundwa 1958 na Ramadhani Mashado Plantan, Abdulwahid
Abdulkarim, Hamisi Hunde
na Abdallah Mohamed watu ambao hawakuwa
na ushawishi mkubwa katika siasa za wakati ule ukimtoa Mashado Plantan.

Hayo mengine sijaona haja ya kukujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…