Tamu na chungu baada ya kujiunga na forever living products

Biashara hii inatakiwa uifanye kwa watu wenye uwezo sio uswahilini, na ili uifanye kwa wenye uwezo lazima ufanane nao ili wakuamini.
 
ila sio lazima ununue bidhaa, unaweza unatafuta mteja kwanza ukimpata ndio ukanunua kwa pesa yake


Kipengele kumpata Sasa, na Kama ukiweza kuwapata mwanzoni basi hata huko mbele kutoboa ni simple tu
Kama unanunua bidhaa ambazo haziuziki, tafsiri yake ni kuwa FLP wanaoverprice hizo bidhaa, na hapo ndio wanapotajirikia na kukufanya wewe uwe mtumwa wa kuleta mteja mwingine ili wao wanufaike zaidi, huku wewe ukipozwa machungu kwa pesa kidogo ya kamisheni. Kama nimeelewa sasa.
 
Hili neno "bidhaa" ama "product" linatakiwa kutolewa elimu yenye ufanisi ya kutosha.

Hata wewe mleta mada haujaanika mtiririko wa aina ya bidhaa hizo, ndiyo maana watu wanakuwa na mashaka na wewe pia.

Je bidhaa hizo zinatengenezwa wapi, zinatumikaje, kwa nini ziwe na bei kubwa kupindukia, nk nk?

Hivi kweli kila mtu katika jamii ana uwezo wa kushawishi mteja mnunuzi na kutengeneza profit?

Kungelikiwa na uwazi katika maswali niliyoorodhesha, pengine pasingelikuwa na mtu wa kuweza kushawishika na kuingia kichwa kichwa.

Kutokana na changamoto za kupata wateja na kauli zinazotumika kusarandia wateja, ndiyo maana watu huona na kuconclude kuwa kampuni hiyo ni ya kitapeli 100%.
 
Biashara hii inatakiwa uifanye kwa watu wenye uwezo sio uswahilini, na ili uifanye kwa wenye uwezo lazima ufanane nao ili wakuamini.
Shid
Biashara hii inatakiwa uifanye kwa watu wenye uwezo sio uswahilini, na ili uifanye kwa wenye uwezo lazima ufanane nao ili wakuamini.
Ni kweli kabisa, ni ngumu kumuuzia mtu product ya laki 2 bila kukufahamu
 
Shida ni kwamba hizi products zinatoka Marekani, na kampuni inauza kwa dollars

Shida pesa yetu haina thamani mwisho inaonekana zina Bei kubwa

Kuhusu faida, faida ni kubwa tu

Faida sio ishu, ishu ni kuuza
 
Majibu ya hayo maswali ni Hadi mtu atake kufahamu

Hauwezi kuconclude utapeli wakati hujui hapo utakuwa umbumbumbu


In short Kuna vitabu vyao vinaelezea hayo yote
 
Haina tofauti na wale vijana wanaovaa tai huku wamebeba bidhaa kibao, wanatembeza barabarani,
Ni kazi ya kitumwa sana, kama wanataka kuuza sana kwanini wasitangaze kwenye vyombo vya habari?
 
Kweli katika watu wanne mmoja ni tahira

Inaonekana wewe ni mmoja wapo

Hakuna sehemu nimeandika namtaka mtu na nimeshasema nimeacha kufanya biashara hii na sababu nimetoa
Acha lugha za mstusi.

Katangaze biashara hii kwenu.

Mimi sitaki kusikia habari za Flp
 
Hiyo ni ponzi kama ponzi nyinginezo. Hawana tofauti na Deci. Kinachofanyika uli kuficha udeci wao ni kuingiza product katikati. Matapeli wengi wa pyramid schemes huingiza bidhaa katikati ili waonekane ni biashara ya kuuza na kununua. WNW(Wajinga ndiyo waliwao)
 
Hapo kwenye kuongea sana ndio point kuu! Hiyo biashara ili ufanikiwe unatakiwa uwe mtu wa watu yaani dzain ya mtu ambae ukihamia sehemu ndani ya wiki mbili watu wote mtaani wanakujua kutokana na uchangamfu wako na ku mingle na watu wa aina mbalimbali

Cha kusikitisha sio watu wote tumeumbwa na haiba ya namna hiyo. Hii biashara km unajijua ni mtu wa aibu halafu hujiamini usithubutu hta kuisogelea coz lazima utafeli.

Binafsi hii biashara ilinishinda kwa sababu km alizoainisha mleta mada.
 
Haina tofauti na wale vijana wanaovaa tai huku wamebeba bidhaa kibao, wanatembeza barabarani,
Ni kazi ya kitumwa sana, kama wanataka kuuza sana kwanini wasitangaze kwenye vyombo vya habari?
Biashara ya forever haifanyiki hivyo

Sio biashara ya kutembeza

Ni biashara ya kutangaza kwenye mitandao ya kijamii

Yaani unatumia Facebook , Instagram, you tube nk


Unalipia matangazo (ads)

Tangazo lolote ukilikuta Facebook/Instagram limeandikwa " sponsored" ujue dollars zinahusika
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hapo umeongea ukweli kabisa

Wale wanaojijua ni maintrovert wasiisogelee kabisa hii biashara
 
Nadhani pia ishu sio tu uwezo wa kuongea sana, ishu unaongea na watu gani? Kama wewe umezungukwa na walala hoi hata uongee kutwa kucha ni kazi bure!

Mimi kuna rafiki yangu alikua anafanya hizi biashara, siku hiyo kaniletea boksi la majani ya chai (green tea nadhani) ananiambia shilingi 60,000. Mi nikipiga mahesabu majani ya chai dukani boksi nanunua 3,000 nikamfurusha! Hizi bidhaa ni ghali sana kwa mtu wa kawaida kununua.

Mwisho kingine kinacholeta ugumu ni mtindo wetu wa maisha wabongo kwamba mtu kutumia dawa ni mpaka awe anaumwa hoi, hatuna utamaduni wa kutumia supplements so inakua ni ngumu sana kumshawishi mtu anunue dawa wakati haumwi.
 
Imegombanisha ndugu wengi sana ...maana watu wakiwa desperate kutafuta members wanahamia kuwalagai ndugu zao 🀣🀣
 
Forever sio utapeli, biashara ambavyo inaendeshwa kwenye nchi 150+

Hivi nchi za Asia na ulaya zinaweza kukubali kufanyiwa utapeli??

Hii sio utapeli sema ni biashara ambayo Inahitaji watu wa kipekee kuimudu

Tofauti na biashara za kawaida (commodity business) hii ni expert business hivyo sio kila mtu anaweza kuifanya
 
Acha lugha za mstusi.

Katangaze biashara hii kwenu.

Mimi sitaki kusikia habari za Flp
Sasa Kama unakuja kuchangia mada kipumbavu unataka nikujibu kistaarabu??


Kuna sehemu nimekulazimisha kujiunga au nimezungumzia kujiunga??

Acha kuja kumalizia stress zako jamii forum
 
Jamaa yupo sahihi. FLP ni ponzi iliyojificha kwenye bidhaa hizo. Haina tofauti na deci. Ukishaoina faida yako inatokana na kuingiza watu jua upo kwenye upatu.
 
Apo akuna cha tamu ni chungu tu [emoji2957][emoji2957]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…