Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Kwel kabisa
 
Kama umeajiriwa ishike Ajira yako.
Wazo la kimasikini sana hili, inaonekana wew utaendelea kuajiriwa mpaka unakufa kwa kukosa tu ujasiri wa kujiajiri! Acha kuwa na mawazo mgando kama haya[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimeshaingiza products kama tano hivi sokoni kama mjasiriamali asiye na kampuni ...
Zote zimekufa kuhusu.

Nikafungua mgahawa .. fanta Sana KAZI ... Human resource chamgamoto kwa sehemu nilipo wanaridhika mapema mno mtu akikunja ila 150 a month humwoni tena .

Means inabidi uanze upya.

Ilibidi niingie front me mwenyewe .. niandae ,nitafute orders na nisambaze/nifaye delivery alone .

Mgahawa ukasimama tena nkasema huu ndo wakati wa kuangalia mitikasi mingine ikiwemo kuraise funds za startups zangu nyingiñe ...
Wiki tatu tuu nilimwachia Yule binti mgahawa ukadedi.

Nikaingia kwenye Biashara ya lubricants ... Kifo cha mende nkapigwa mande ...

Nlikuwa na kaeneo kangu nikakauza last year mwishoni bei ya hasara nikaamua kuitumbua .

Sasa hv naandaa proposal kuomba funds Us embassy 😂😂😂😂
 
Unadhani kujiajiri ni matako kila mtu anayo?
Wazo la kimasikini sana hili, inaonekana wew utaendelea kuajiriwa mpaka unakufa kwa kukosa tu ujasiri wa kujiajiri! Acha kuwa na mawazo mgando kama haya[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bosi naomba kazi hautajutia, mm ni mtaalamu wa masoko
 
Niliwahi fuga kuku wa mayai 600, wiki chache kabla ya kuanza kutaga walipata ugonjwa na kufa karibu wote
 
Nilikopa milion 1 nikafungua mgahawa mzuri tu na,yaani kila siku naongeza idadi kuanzia unga,mchele,ngano.

Changamoto ikaja kwa wafanya kazi,yaan nilikuwa nao wadada watatu(3),wale wadada wakawa wameambiana ikifika muda flan basi chakula wasiuze ili waondoke nacho.

Basi chakula kinabaki jioni wanajigawia wanakwenda kula na familia zao,sasa siku moja wateja ndio wakaja kutustua kwamba chakula chetu kinaisha mapema,tena mpaka walishajua muda huu ukienda pale chakula hakuna,kumbe kipo ila wanataka warudi nacho.

Nilifukuza wote sikuonea huruma mtu,moja ya changamoto kubwa na hasara ilinifika hii
 
Mimi biashara yangu ya production kuna siku mzigo uliharibika kilo 200 za scrub kwa kikosa kidogo sana aysee sikukanyaga kiwandani wiki nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…