Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Ndugu @kichangirl, hongera sana kwa hatua hiyo,mm namiliki mawazo kama matatu hv ambapo kabla ya mwaka kuisha mawili yatakuwa yameshaanza coz mtaji ninao tayari ila kiukweli haya mawazo nimeyachakata kweli na nimejipanga kisawasawa.Hapo kwenye viazi mabibo ni biashara ambayo naiadmire sana coz mwakani nafumua kama ekari 5 za viazi coz nishagain experience ya kutosha in this field,ila nitataka nipate connection ya wanunuzi au madalali hapo mabibo,kwa kuwa upo hapo dar na ulishapita mitaa ya mabibo sokoni,nikuombe tu bibie kama unaweza wa kunitafutia mawasiliano ya watu wanaodeal na hii kitu kwa ajili ya maandalizi ya mapema ya soko mwakani.
 
Mim nakumbuka siku ya kwanza nafungua biashara yangu nilipata wateja 5 siku ya pili nilipata mteja 1 ilinichukua km miezi3 mpka kuanza kuchanganya nimshukuru mungu Leo Nina miaka7 kwenye hii biashara Nina nyumba 2 hapa mjin na kiwanja
 
Okay mi ni ME sio bibie. Nakutumia namba ya dalali mmoja PM ni mshkaj mwelewa mcheki unaezapata ABC za sokoni kutoka kwake
 
Kumradhi sana @Kichangirl kwa kudhani ww ni KE kumbe ni ME,nilidhani girl ya mwishoni kwenye id yako inamaanisha jinsi,all in all thanx for your support.
 
Ndugu mkewangu ni mrokole ana imani kali sana anasali karibia siku zote za week, hata chanzo cha kufilisi duka ni sababu alikuwa anafungu muda mchache muda mwingi yuko kanisani

Ulimuoa akiwa mlokole au ameokoka ndani ya ndoa?
Kama ni ndani ya ndoa mpige stop huo ukichaa wewe ni kichwa cha familia hakuna kinachokushinda hapo
 
Mim nakumbuka siku ya kwanza nafungua biashara yangu nilipata wateja 5 siku ya pili nilipata mteja 1 ilinichukua km miezi3 mpka kuanza kuchanganya nimshukuru mungu Leo Nina miaka7 kwenye hii biashara Nina nyumba 2 hapa mjin na kiwanja
Unaweza kunijuza hiyo biashara mkuu?
 
Biashara mbaya toka mwezi 7 na mwezi ujao natakiwa nilipie kodi ya flem
Akiba sina ,bidhaa zimepungua ,pesa ya kuongezea bidhaa sina

Huwa inafika muda natamani hata ningeajiriwa tu,
Nikasubiri hiyo pesa ya mwisho wa mwezi.
JAMANI KUJIAJIRI KUNA CHANGAMOTO KUBWA.
 
Nakushauri kabla hujaamua kuwavaa madalali moja kwa moja ni bora uende mwenyewe kwenye masoko ya viazi na ujifanye 'dalali' kuwa eti tayari una mzigo wa viazi kwa bei ya 000 tshs utakaopatikana tarehe x. Halafu chukua na mawasiliano yao hao wauzaji. Mimi niliwahi kufanya hivi kipindi namsaidia mjomba kuuza nanasi kutoka kiwangwa bagamoyo na kuzileta mjini. Madalali wa kibongo ni wakandamizaji sana. Walishangaa Canter inashusha mzigo bila wao kujua na unauzwa fresh tu.
 
Nilianzaga biashara ya mpesa huko vijijini nkamuweka wife changamoto take ni chuma ulete mingi sana ukipata faida laki 4 wao wanachukua lak6 sio mchezo mpaka nilifunga

Ila ntarudi tena kuifanya kwan inalipa sana
 
NENDA KAAJIRIWE.
 
Kumradhi sana @Kichangirl kwa kudhani ww ni KE kumbe ni ME,nilidhani girl ya mwishoni kwenye id yako inamaanisha jinsi,all in all thanx for your support.
Wewe ndiye unakosea kuisoma Id yake...ni Kichangiri na siyo Kichangirl. Id yake haina neno "girl"
 
Mkuu umetoa hamasa kubwa sana na funzo ndani yake,hongera kwa kua na msimamo na kutambua nn unataka maishani.
 
Ukiskia wapambanaji bhasi ndio kama weae mkuu
 
Ukawa unajiuliza watu wote hawa wanakuja kariakoo na sipati mteja hata mmoja wa kutoa hela.Hongera mkuu Mungu atafungua njia mambo yatakaa sawa
 
Kuna rafiki yangu alikua anatoa mkaa hukohuko iringa kuleta dar,kilichomkwamisha ni dhuruma za madalali.
 
Kikubwa katika dunia hii hakuna biashara ambayo hailipi....Maisha ya binadamu na viumbe vingine ili yaende yanahitaji matumizi ya bidhaa...fikiria mtu anaagiza contena ya vijiti vya kusafishia masikio au kusafishia meno anauza na vinaisha....wengi tunaanza biashara bila kufanya utafiti wa kutosha wa mahitaji ya soko....mtaji unaohitajika....bei ya kuuzia na kununulia...eneo la kufungulia biashara... uvumilivu ni wa muhimu sana...biashara nyingi sio rahisi ukafungua leo na kupata faida...inahitaji muda kwani wakati unaifanya ndio pia unajua vitu ambavyo mwanzoni ukuvijua...biashara ni kitu hai ... ni kama mtoto...anaziliwa ..anakaa...anatambaa...usimamizi wa biashara pia ni muhimu sana...Niliwahi kwenda Guangzhou baada ya kupata maoni hapa Jf....nilipofika sokoni nakuta bei ya bidhaa nilizohitaji ni kubwa kuliko hata hapa kariakoo...kwa kweli nilichanganyikiwa sana...na huku niliambiwa wewe nenda tu bei ni rahisi sana.
 
Kuna mazingira mabaya ya kibiashara ndani ya hii nchi.Msihangaike kumtafuta mchawi.
 
Sawa sawa, nimekusoma mkuu kwa ufafanuzi zaidi ulioleta.
 
Biashara ni sayansi pana ukiweza kuwa mvumilivu ukaweka umakini na juhudi lazima utoboe ..maana utakuwa ume master mbinu za close deal na customer wako

Mkuu jitahidi ukimbazane na mauzo uza uza uza
Umenena vyema, biashara ni mauzo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…