Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Chama cha Waandishi wa Habari Wananawake (TAMWA Zanzibar) kinawashauri wanawake wa vyama vyote vya siasa kujitokea kwa wingi katika kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali ndani ya vyama vyao.
Ushauri huo unakuja siku chache baada ya vyama vya siasa kutoa nafasi kwa wanachama wao kuwania nafasi mbali mbali kuchukua fomu za kugombea katika nafasi tano za uongozi Tanzania, ikiwemo ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Zanzibar, Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Udiwani; Zanzibar kama sehemu ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
“Tunawashauri kutobaki nyuma na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo tunawaomba wanawake mjitokeze kuwania nafasi hizo za uongozi” alisema taarifa ya Mkurugenzi wa Chama Cha Wananchi Habari Wanawake Tanzania kwa upande wa Zanzibar Dk Mzuri Issa.
Imeelezwa kwamba kwa mujibu wa Sensa ya idadi ya watu na makaazi ya mwaka 2012 Zanzibar ina idadi ya watu wapatao 1,303,569 na kukisiwa kufikia 1,671,598 kwa mwaka 2020 ambapo wanawake ni zaidi ya asilimia 50.
“Hata hivyo uwingi huo wa wanawake hauendani na nafasi zao katika vyombo vya kutunga sheria na kufanya maamuzi na wakati mwingi wanawake hao huvunjwa moyo na kupikiwa majungu kwa makusudi wakati wa kugombea nafasi hizo ili hali hiyo isibadilike” Ilisema taarifa hiyo ya TAMWA.
Aidha kutokana na mazingira hayo, Dk Mzuri amesema ni wastani wa wanawake 200 tu ndio walioteuliwa na vyama vyao kwa Zanzibar kugombea katika maeneo hayo matano ya uchaguzi ya mwaka 2015 ambapo kwa nafasi ya Urais iliendelea kutokuwa na mwanamke tokea kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mnamo mwaka 1992.
“Tunawaomba wanawake wajitokeze kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba na pia kuwaongoza wananchi katika nafasi mbali mbali sambamba na wenzao wanaume” alisisitiza Dk Mzuri.
Chama cha Waandishi wa habari Wanawake (TAMWA) kimekuwa kikitoa mafunzo kwa wanawake wanaotaka kutia nia na kuwajengea uwezo wa kujiamini ili waweze kupambana kwenye kinyanyanyiro cha kuwania nafasi mbali mbali za uongozo kupitia vyama vya siasa.
Hata hivyo Dk Mzuri amesema ni kawaida, wanawake kuelekezwa kugombea nafasi za viti maalum tu ambavyo kijinsia huwa havioneshi usawa wa kijinsia na umoja wa wanawake bali huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta mgawanyiko wa wanawake.
Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ni wanawake watatu tu ndio walioweza kuchaguliwa kupitia kwenye majimbo katika nafasi za ubunge sawa na asilimia 6, wawakilishi saba sawa na asilimia 14, madiwani 23 sawa na asilimia 20 na nafasi ya Uraisi ambayo ni moja tu imeendelea kushikiliwa na mwanamme.
“TAMWA Zanzibar pia ingependa kuishauri jamii kuwaunga mkono wagombea wanawake ili waweze kuonesha uwezo wao na hivyo kuleta uwiano katika jamii pamoja na maendeleo kwa ujumla” imesema taarifa hiyo.
Sambamba na hilo TAMWA pia imeiomba na kuisisitiza Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuweka mfumo maalum wa kupokea maoni kutoka kwa wananchi hasa wanawake wanaokumbwa na udhalilishaji katika kipindi hichi cha heka heka za uchaguzi zinazoendelea nchini.
Wakati vyama vyengine vya siasa vikiwa havijaanza kutoa fomu za kuwania nafasi za uongozi tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kutoa fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Kwa upande wa Tanzania hadi sasa ni Dk John Pombe Magufuli ambaye anatetea nafasi yake katika kipindi cha pili cha uongozi huku kwa upande wa Zanzibar waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za Urais wa Zanzibar jumla yao ni 11 akiwemo Mwanamke mmoja tu naye ni Bi Mwantum Mussa Sultan.
Wengine waliojitokeza kwenye kinyanganyiro hicho ni Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed Jaffar Jumanne, Mohammed Hijja Mohammed, Issa Suleiman Nassor na Makame Mnyaa Mabarawa Mbwana Bakari Juma.
Wengine ni Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa na Hussein Ali Mwinyi.
Uchukuwaji wa fomu umeanza wiki hii na zoezi hilo litaendelea hadi Juni 30 na kufuatiwa na vikao vya CCM kupitisha jina moja la mgombea atakayemrithi Dk Shein akishinda urais wa Zanzibar katika uchgauzi wa mwezi Oktoba mwaka huu.