TANAPA ni shirika kubwa sana linakusanya pesa nyingi kupitia Mlima Kilimanjaro ila cha ajabu ni kwamba, waliokwenda kuzima moto mlimani ni waliambiwa wawe watu wa kujitolea ambao walikusanywa Mgambo wa Kilimanjaro na Arusha hawa ni miongoni mwa waliokwenda kusaidiana na wengine kuuzima moto, sasa watu hawa wanaingia kwa shift kutoka chini kupanda mlima ambapo moto ulipo wanatumia masaa 3 na zaidi.
Mfano kuna group linaingia shift ya saa 12 jioni wanatoka saa 3 asubuhi cha ajabu kila mtu anafungiwa mikate mikubwa 3 au 4, soda ndogo ya portable 1 ya sh 500 na glucose ya kulamba basi hakuna chakula kingine. Hivi kweli hawa viongozi wanawaonaje hawa watu wa kujitolea wa kuzima moto hicho ni chakula? Chakula hicho na baridi uliyopo kule juu unaweza ukakaa nacho hadi saa 3 asubuhi?
Moto wanazima kwa majani unakata majani unapigapiga ndio uzime kweli are we serious TANAPA wameshindwa kukodi ndege za zimamoto ukizingatia ule moto ni mkubwa na unasambaa kwa kasi sana, mmeshindwa hata kuwapa mama ntilie tenda wawapikie ugali nyama kweli? Hakuna cha posho au incentive yoyote baada ya hapo utaambuliwa tena usafiri urudishwe walipo kuchukua, hapa ni kupimana uzalendo au.
Jana kuna mmasai mgambo walipomaliza tu wakarudi, ilipofika saa 1 jioni wakapigiwa simu kuwa moto umeanza tena warudi, kwani walikubali kurudi? Huenda wachache walirudi ila walio wengi wamekataa. Mabilioni inaliwa na wengine na wengine ndio wakufanya kazi za kujitolea.
EH MUNGU TUSAIDIE