Tanbond aimepotelea wapi?

Tanbond aimepotelea wapi?

Kisanduku

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2009
Posts
284
Reaction score
483
Naamini swali langu litajibiwa,

Nimekulia Mwanza utotoni na ukubwani nikahama kutafuta maisha kona zingine za nchi. Ninakumbuka wakati fulani hapa nchini kulikuwa na mafuta ya kupaka kwenye mkate yaitwayo TANBOND yaliyokuwa yakitengenezwa hapa na kiwanda kilichopo Mwanza kiitwacho VOIL.

Kuanzia mwaka 1986 kidogokidogo yakaanza kuingia mafuta kama yaleyale yakitokea Kenya yaitwayo BLUE BAND.

BLUE BAND ikachukua nafasi kidogokidogo na TANBOND ikaanza kupotea kdogokidogo. Leo hii niko kimatembezi hapa Mwanza naulizia wenyeji wa hapa kumbe hata baadhi hawajui kama kulikuwa na TANBOND!

Nilishangaa kwani nilijua hata miko mingine iliijua TANBOND ya Mwanza. Niliyemuuliza akajitetea kwamba si kila familia ilikuwa na uwezo wa kununua TANBOND.

Mimi nikambana kwa kumkumbusha kuwa enzi za utoto tulikuwa hata tunaokota makopo jalalani na kuyachezea kuunda magari hivyo lazima kopo la TANBOND utalikuta tu.

Maana si TANBOND tu iliyopotea bali hata mafuta ya kupikia SUPA GHEE yaliyozalishwa na VOIL ileile nayo hayaonekani.

Hata kile king'ora cha kila saa nane mchana au saa nne usiku kilichoashiria wafanyakazi wa shift wa pale VOIL kutakiwa kazini hakipo. Kilikuwa kikipigwa basi sehemu kubwa ya Mwanza ilikisikia.

Hakika kiwanda hiki unaweza kusema kimekufa japo sijafanya utafiti zaidi ya huo.

Dhana yangu ni nini? Je, vitu hivi ndivyo vinatufanya tuwaogope wakenya?
 
Mkuu TANBOND ni bora saaaana tu kuliko hii Blue band yao. kwa sasa ukija Dar utaikuta Mlimani city pale SHOPRITE. mwanangu akitumia Blue Band anapata allergy vipele vinamtoka so dokta akatushauri tutumie TANBOND. sasa hivi package yake ipo kwenye vikopo vya plastick km Blue band ila wengi wa wa TZ wa sasa hawaijui ile kitu bana. tehe nakumbuka home ilikuwa ikinunuliwa kwa sana tu basi ikiwekwa kwenye mkate utajing'ata si mchezo baba.
 
Ipo mkuu. Hata hapa ninakopata soda mida hii kuna hii kitu TABOND kwenye kopo la plastic la rangi ya njano kwa package ya 250gms, 500gms na 1kg. Inazalishwa na Vegetable Oil Industry Ltd, P.O box 1211 Mwanza. Inawezekana nabii hakubaliki kwao.
 
kaka mzigo wa ukweli huu naukumbuka sana miaka hiyo ya enzi za mwalimu, tatizo hawa jamaa hajitangazi kabisa, kizazi hiki cha dot com biashara matangazo, au ndio mipango ya wenzetu kutumaliza kiaina?
 
da jamani kupatikana kwa TANBOND ni kwa shida na sana mpaka najiuliza kama kiwanda kipo! kutangazwa haitangazwi hakuna promosheni yoyote ndo maana vijana wa sasa hawawezi kuijua
 
Nilikuwa naipenda sana TANBOND, kitambo sijaitumia ila mzuka umenipanda ghafla lazima niitafute sijui kama huku Mtwara inapatikana
 
TANBOND ipo, tatizo la VOIL kwa sasa nadhani ni management mbovu na mambo kuendeshwa kihindihindi! naskia pale sku hizi wamebezi sana kwenye mafuta ya alizeti (yasiyokuwa refined) na kutengeneza vitu vya plastic!..nadhani hivyo ndy vyenye wateja! Mimi natumia TANBOND toka miaka ileeee, sku hizi upatkanaji mpaka mjini tu!
 
TANBOND ipo - Tatizo inapatikana kwa uchache sana - probably watengenezaji wanakwepa gharama za usambazaji!

Watoto wengi waliozaliwa 80s na kuendelea hawajui TANBOND! Kwahiyo usishangae sana ukimwuliza mtu wa miaka 30 kuhusu TANBOND akakwambia haijui.
 
naipenda sana TANBONND haina athari yoyote kwa ngozi yangu tofauti na blueband ila kwa miaka ya hivi karibunu haipatikani kwenye maduka ya mtaani.Nafikiri production yake ni ndogo
 
Back
Top Bottom