Naamini swali langu litajibiwa,
Nimekulia Mwanza utotoni na ukubwani nikahama kutafuta maisha kona zingine za nchi. Ninakumbuka wakati fulani hapa nchini kulikuwa na mafuta ya kupaka kwenye mkate yaitwayo TANBOND yaliyokuwa yakitengenezwa hapa na kiwanda kilichopo Mwanza kiitwacho VOIL.
Kuanzia mwaka 1986 kidogokidogo yakaanza kuingia mafuta kama yaleyale yakitokea Kenya yaitwayo BLUE BAND.
BLUE BAND ikachukua nafasi kidogokidogo na TANBOND ikaanza kupotea kdogokidogo. Leo hii niko kimatembezi hapa Mwanza naulizia wenyeji wa hapa kumbe hata baadhi hawajui kama kulikuwa na TANBOND!
Nilishangaa kwani nilijua hata miko mingine iliijua TANBOND ya Mwanza. Niliyemuuliza akajitetea kwamba si kila familia ilikuwa na uwezo wa kununua TANBOND.
Mimi nikambana kwa kumkumbusha kuwa enzi za utoto tulikuwa hata tunaokota makopo jalalani na kuyachezea kuunda magari hivyo lazima kopo la TANBOND utalikuta tu.
Maana si TANBOND tu iliyopotea bali hata mafuta ya kupikia SUPA GHEE yaliyozalishwa na VOIL ileile nayo hayaonekani.
Hata kile king'ora cha kila saa nane mchana au saa nne usiku kilichoashiria wafanyakazi wa shift wa pale VOIL kutakiwa kazini hakipo. Kilikuwa kikipigwa basi sehemu kubwa ya Mwanza ilikisikia.
Hakika kiwanda hiki unaweza kusema kimekufa japo sijafanya utafiti zaidi ya huo.
Dhana yangu ni nini? Je, vitu hivi ndivyo vinatufanya tuwaogope wakenya?