Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama 14 Vikuu vya Ushirika vya Pamba, (Tanzania Cotton Co- Operatives Joint Enterprise Limited-TANCCOOPS LTD), wamekutana Mkoani Shinyanga huku wajumbe wa Mkutano huo wakitakiwa kuwa na uchungu na chama hicho, ili kujenga ushirika ulio imara zaidi na wametakiwa kujisimamia na kuendesha ushirika kibiashara.
Hayo yote yamedhibitika katika Mkutano Mkuu wa TANCCOOPS LTD, uliofanyika katika Ukumbi wa Shirecu1984 Ltd, ambao katika Mkutano huo Mgeni rasmi ni Mrajis Msaidizi Bi. Grace Mwagembe ambaye alimuwakilisha Mrajis kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania na kuhuzuliwa na wajumbe wa TANCCOOPS LTD, inayoundwa na Vyama Vikuu vya Ushirika 14 kutoka katika Mikoa inayolima zao hilo la Pamba.
Licha ya kujadili mambo mbalimbali yatakayochangia kuimalisha Ushirika, pia katika Mkutano huo kulifanyika uchaguzi wa kuziba nafasi zilizokuwa wazi,na kuchaguliwa wajumbe wa wili wa Bodi na wawakilishi moja wa nje ya Bodi ya TANCCOOPS LTD, katika uchaguzi huo, Ndg; Baraka Joseph Masoko wa Mirambo Union na Lazaro Kidaiga Walwa, walichaguliwa kuwa wajumbe wa Bodi na Ndg; Daniel Mwita Masanja, kuwa mjumbe wa nje ya Bodi.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Bi. Grace amesisitiza kuwa endapo mjumbe wa Bodi ataenda kinyume na matakwa ya Ushirika, basi ajue atakaa pembeni na nafasi yake itajazwa na mtu mwingine na wajumbe waliochaguliwa watapewa mafunzo elekezi.
Eidha amesema kwamba Ushirika ni biashara, hivyo amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuwa wabunifu wanapoongoza wenzao, hasa kuwa na uchungu na chama ili kujenga Ushirika ulio imara, na wajue tasnia ya Pamba inavyokwenda na mnatakiwa mjikaze zaidi na mjiendeshe kibiashara.
"Ninawaomba msichukulie Ushirika kuwa kitu cha kawaida, msijifanye wajuaji sana kwenye mambo msiyoyafahamu mkaharibu mambo, tunataka ushirika biashara, naomba pia mhamasishe wanawake wengi kuingia kwenye Ushirika, kwani waliopo ni wachache sana" alisema Mwagembe.
Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu, Kwiyolecha Nkilijiwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirecu1984 Ltd, amewataka kuacha mara moja wale wenye tabia za kuwachafua baadhi ya watendaji, kwa kuwa wao hawajapata ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza vyama vya Ushirika.
"Tunataka tuondoe makundi katika vyama vya Ushirika, wamo baadhi ya watendaji ambao wametokana na makundi ya watu au Makampuni, ambao wapo kwa maslai binafsi na sio maslai ya Ushirika" alisema Kwiyolecha.
Hata hivyo kwa upande wake Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza katika mkutano huo Mkuu, amesema ushirika ni ushindani kwa hivi sasa, hivyo ni lazima ushirika ujiendeshe kibiashara, yale mambo ya kiholela hivi sasa hayapo.
"Shindaneni kibiashara hakuna mtu wa kukubeba, ukilia utalia kivyako, jipange kibiashara yale mambo ya kwenda kiholela hayapo tena, tunatakiwa kubadilika na tufanye ushirika kwa umakini" alisema Bi. Hilda.