TANESCO board split on MD Rashidi's fate


Rhetorics
 
Zitto ndugu yangu sawa inawezekana anafaa ila tutaishije na doa la RADAR? Mbona tumeshindwa kuishi na doa la RICHMOND tukamvua Uwaziri Mkuu mtu ambaye wadau wanakiri ni mtendaji wa hali ya juu? Unataka kusema LILA na FILA sasa VINATANGAMANA?

Ufisadi wa RADAR kwa mujibu wa makaratasi ya SFO unajadiliwa JF? Au ndio hukumu tayari?
Akamatwe akajibu mashitaka yake huko. Swali litakuja nani amkamate, wananchi tuna nguvu za kusukuma DPP kufungua mashtaka dhidi ya watuhumiwa. Mwishowe itakuwa yale yale ya kila mtu fisadi (unaona hata Sopshia Simba anaona eti michango ya harusi ya ya Jeetu Patel ni ufisadi wa Anna Kilango ili mradi tu kila mtu avikwe shuka ya ufisadi). CEO wa TANESCO sio mwanasiasa, ni mtendaji na hivyo hakuna kilichoitwa ajali ya kisiasa.......!!!!!!!
Tunapogeuza ufisadi ni mijadala ndio tunapoenda mrama. Mpaka sasa ni tuhuma na mahakama ikimtia hatiani hutaniona ninajenga hoja hizi. Lakini kama kuna ufisadi, au tuhuma za ufisadi akafanya TANESCO toka amekuwa CEO pale ziwekwe hapa na sio kutumia visingizio vya SFO kumhukumu mtu katika court za vijiweni.

Kuna vested interest nyingi katika Mashirika na kuna watu wanaona ni zamu yao kula. Ni suala la kuchagua nani iwe zamu yake maana siku hizi media ni silaha za wazi na kila kundi lina media zake. Katika TANESCO kuna zaidi ya tunachosoma katika This Day na Kulikoni au gazeti lingine loote. Kuna watu wanajaribu kuwatake wengine for granted. Wanaweza kufanikiwa lakini maana siku hizi Tanzania ni 'either with us or with Fisadis'
 
Wizi wote unaotokea huwa ni siri mpaka bomu linapolipuka, wakati wa Rashid akiwa gavana wizi wa epa ulikuwepo na hata kuna mwanahalisi alishatoa moja ya wizi wa EPA enzi za Rashid akiwa gavana na fungu hili lilipitia Akiba Benki na nakala yake ilikuwepo kwenye mwanahalisi, So Rashidi si safi hata kidogo ni fisadi
 
Rhetorics

Rigidity..! Hebu tupunguze.

Tunasema mzuri, hajawahi kutokea, n.k.
Nadhani ni kiwango cha ufahamu tu. Kama hujawahi kuona mambo yakienda vizuri zaidi ya hapo, huwezi kuona ubaya. Lakini kwangu mimi nimeona mashirika yeaendayo vizuri duniani na CEO wazuri, wengine ni wa-TZ

Rashid can’t be a subset of them. Tatizo ni hizo support zisizokuwa na objectivity. Zimejaa siasa. Tulisoma naye, tunamfahamu, alitoa allowance nzuri, n.k, n.k
 
Pre-emptive strategy...........!

Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals.

Lets not lose sight here as to what is at stake... ITS INTERGRITY.
Dr Rashid experieced,learned or otherwise has not proven his worth.
When you have carry on baggages like the RADAR scandal and the Serious Fraud Office(SFO)is hounding you, is not exactly one thing to be proud of.
Dr Rashid has not proven to be a character of the caliber of Mr Arnold Kilewo,Mr Mbowe(formely of TIB), Mr Nsekela etc.

Ill intentions in management can kill ones reputation, as is the case with Dr Rashid
 

hebu thibitisha na habari za mwanahalisi zithibitshe kwa kutueleza namba ya toleo la gazeti. Habari zilizopo mpaka sasa ni zilizotolewa na Raiamwema kwa vithibitisho kwa EPA kuanza mwaka 2000. Ni kweli kulikuwa na debt conversion schemes etc. Thibitisha ufisadi uliotokea huko na tutakubaliana nawe badala ya kutoa sweeping statements.

Halafu tutaenda nyuma kuanzia kwa Mzee Mtei mpaka kina Nyirabu, Rutihinda nk ili kuona hizi schemes zilikuwaje. Pia tutaangalia wakati Benki Kuu inaungua ilikuwa ni nini nk. Yaani tuanze toka wakati wa Mwalimu akiwa Rais na hatua alizochukua, kwa mfano kwa kuungua Benki Kuu. Tusiwe na memory ndogo kwa ajili ya kumhukumu mtu.

On RADAR - nimesema hili ni suala la mahakamani na tushinikize wanaotajwa wapelekwe mahakamani na mahakama ndio pekee zenye mamlka ya kusafisha mtu au kuhukumu. Ingawa najua zitakuja hoja za uhuru wa mahakama nk - maana hata mimi suala la Zombe liliniacha hoi licha ya kuheshimu uhuru wa mahakama.
 

nipo flexible katika hili. Nipe facts tu na nitakubaliana nawe.

Sijasema hajawahi kutokea
 

Integrity nakubaliana na wewe 100%! Mahakama basi ifanye kazi maana tusiwe mahakimu ingawa kuna court of public opinion.

Sina comment on kina Kilewo maana ni watu ninaowaheshimu sana ingawa nao wana mawaa yao. Tulikodisha KIA kwa kampuni ya kiingereza kwa tozo la dola 1000 kwa mwaka na kampuni hiyo mdau wake ni Mzee Kilewo. Unakumbuka lawama kwa Nsekela on ukabila nk. Ndio maana huwa sipendi kuhukumu watu kwa jumla jumla
 

Sawa sawa Mkuu Zitto, lakini allegations za Dr Rashid zinagusa moja kwa moja kwenye maamuzi yake ambayo ni fraudulent in nature.
Hivyo basi reputation ya mtu kuongoza kitengo chochote cha kibiashara inakuwa na walakin, na anporudishwa mahala hapo against public opinion eyebrows tend to be raised.
Hivyo basi inabidi wasi wasi huo uondolewe na mahakama KABLA ya mtu huyo kupewa madaraka mengine kama hayo.
Hao nilio wataja hawakuwa DIRECTLY implicated katika allegations ulizozitoa , bali ni third party.
 
 


This is very well said Mkuu, Asante sana na hili ndiyo tatizo kubwa la viongozi wetu. Na ndiyo maana wanaonekana waganga njaa!
Wengi wamo kwenye viti vyao ilimradi liende No satisfaction, completely zero achievements, wanapokea watoto wa wakubwa na kuwapa kazi hata kama hawana sifa. Ni wakati gani watoto wa vigogo walikuwa recruited sana pale BOT?? A mess they are struggling to clean now! Tusitetee marafiki kwenye kujadili maswala ya kitaifa, wacha uhusiano wako na mtu unapojadili mambo yaliyo muhimu na yanayomgusa kila mtu kwenye Taifa zima. Kama watu hawana uvumilivu wa ku-serve the public as an honest civil servant, with integrity should resign and join the private sector.
Warwanda wameshatuacha, wakenya wameshatuacha, sasa tunangoja wakongo sasa hivi watarudi hali ya utulivu nao pia watatuacha tunapiga bla, blaaa isiyojenga nchi yetu.
 


Mjomba hayo majina una uhakika na unavyo visema?
Fanya utafiti utajua huko Jersey kuna account ngapi.....
 

Can this 'not guilty until proved in a court of law' conclusion of yours be extended to Chenge who, as the then Minister responsible for Construction, 'constructed' that road in your Kigoma North Constituency?
 


Muheshimiwa, naona kama unateleza kidogo maana hawa wengine umewavalisha kofia haraka ila Dk unamkingia kifua.

Ukweli ni kwamba Dk ni msomi anayekubalika pia ni mchapakazi anayejua afanyalo ila tatizo linabaki pale pale...Accountability.

Je tumpe pass kwa sababu mahakama haijamuhukumu?......
 
Naungana nawe, nchi yetu imejaa majungu kuliko uhalisia. Wakati huyu bwana anachukua shirika jiulize lilikuwa linapata loss kiasi gani? Imagine sasa hivi linakaribia ku brake even. Lini hiyo imetokea? Shirika linakopesheka sasa hivi. Suala la mgawo wa Umeme kwa hali shirika lilivyokuwa lisingeweza kumalizika ndani ya kipindi kifupi hiki maana alilichukua lipo hoi. Mgawo wa Umeme zinahitajika jitihada kubwa zaidi na si za TANESCO peke yake kwa kuzingatia lilipokuwa.
 
Double digit haijachangia na umeme pekee kama unavyodai. Uganda na Kenya ni umeme? Huoni kwamba hizo nchi zipo correlated na Tanzania. Hali ya chakula kwa kiasi kikubwa ndio imetufikisha hapa na kuyumba kwa soko la dunia.
 

Ukiweza kusoma btn the lines nakuwa burudani sana kwani you can see the whole picture.

1)Moja kama nilivyoweka kwenye red highlights,Rashid alidhani kazi yake aliyopelekwa kuifanya imekwisha,he was wrong kwani mambo yalibadilika....Naamini kuwa yalibadilika kwasababu inavyoonyesha kwenye highlights namba..

2)Kuwa aliajiriwa makusudi ili kuja kusawazisha issue za kina Richmond AKA Dowans.

3)Inawezekana weakness zake ndio nguzo kuu muhimu ya kung'ang'aniwa na status quo.
4)Ni yao ilikuwa ni kuuwa issue ya Richmond na alishasema mwanzoni kabisa kuwa yeye hawezi kulaumiwa,inadaiwa hataki politics,lakini anacheza politics,kwa kutotaka kulaumiwa na huku ukweli huu umeonyesha ana msimamo gani na ni kwanini status quo bado wanamuhitaji...

Rashidi is also widely believed to have "displayed major leadership weakness", in the words of another government insider, in pushing so hard for the purchase of rusty power generators from Dowans Holdings AS which inherited the Richmond contract.

"Merits" amabazo zimemconvince board chairman Ngumbulu kumu endorse kwa mara nyingine tena....
Kwa kifupi there is something in common for those who wants Dr Rashid back,something to do with the status quo.
Kaazi..
 
Huu utetezi anaoufanya muheshimiwa kabwe unaonyesha kuwa kuna mengi yamejificha nyuma ya hili sakata la Tanesco na Rashidi. Ni wazi kuwa kwa nafasi yake kuna mengi anayajua ingawa hapa anakuwa mnyimi kutumwagia. Muheshimiwa tuambie nini kinaendelea huko maana tumechoka na hii tabia ya kuchaguliwa kila kitu na magazeti yaliyojaa vibaka wanaosubiri zamu yao nao wawe mafisadi.

Mimi siku hizi nimepata allergy na magazeti ya kitanzania. Imefika hatua wamiliki na waandishi wao wanajifanya kuwa ndio wenye akili kuliko watanzania wote kuanza kuwachagulia kuanzia nani ashike madaraka yale, nani ni mwema na nani mbaya jukumu ambalo hata mitume ya wazungu na waarabu iliwashinda, hadi sasa wanadai kuwa wao ndio wanajua nini iwe ajenda ya taifa letu.

Sasa waheshimiwa kama huyu Mheshimiwa Kabwe anapokuja hapa ni wajibu wake kutupa ukweli wote na sio kutudondoshea vichengachenga tu hapa.

Mheshimiwa ujana dawa ya longolongo la wazee. Tuambie nini kinaendelea huko Tanesco na huyu rashidi. Kwa nini unadhani ni bora kuwa naye yeye kuliko hao wengine wanaotakiwa wawe na hizo vested interests?
 
Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?

Tunaendekeza ukada wa CCM ktk utaalamu ndo maana nchi haiendi popote. Board ya shirika kama TANESCO inatakiwa iwe na members ambao ni wahandisi, wachumi, wanasheria basi. Sasa ukiangalia members wengi wa bodi za mashirika mengi ya umma unakutana na vihiyo kibao.
 
Mjomba hayo majina una uhakika na unavyo visema?
Fanya utafiti utajua huko Jersey kuna account ngapi.....

Mwaga data mkuu,huna haja ya kuhold back, mie niko bongo si Jersey.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…