TANESCO DODOMA.WANANCHI TUMEWAKOSEA NINI..?

TANESCO DODOMA.WANANCHI TUMEWAKOSEA NINI..?

Sela Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,120
Reaction score
7,317
Wakuu kwanza salamu sana. Nipo Dodoma Kwa wiki mbili sa hivi . Lakini Dodoma niliyomo umeme wa uhakika hakuna. Dodoma muda wowote umeme unakata.
Kutoka tarehe 24 hivi Kila ikifika saa sita saba hivi umeme unakatika na kuwaka si chini ya mara 10 Kwa saa Moja. Paap unakuja, paap unakata. Juzi simu yangu ndogo iliungua. Nikatoka mlio ndani Kwa ndani. Jana usiku hali imejirudia ni kata , rudisha mpaka nikaanza kuona aibu!
TANESCO hamna asiyejua mitambo huwa inaharibika but tuambieni kwamba usiku ndio huwa mnatengeneza ili mzime kabisa tupate majibu..sio hiki mnajaribu kufanya.
Ni aibu kwamba mmekuwa chanzo Cha matatizo mbalimbali ya vifaa vya wananchi wanaolipa Kodi kupata huduma.
 
Poleni sana. Tatizo hapo huyo regional
Manager ni kimeo, ni mtu wa majungu majungu na hujuiona anaweza kazi. Yaani kwa ufupi huyo regional manager afukuzwe mara moja
 
kigamboni sasa mchana upo vizuri ikishafika usiku tu. unakata unarudi unakata unarudi hata mara 20.sasa huwa sielew hilo tatizo na watu wanapata hasara vitu vinaungua
 
Hali inazidi kuwa mbaya usiku wa Leo Dom umeme umekatika mara 12 Kwa hesabu ndogo. Pap unakata, paap unarudi
 
Back
Top Bottom