TANESCO emergency Tabata mnakera

TANESCO emergency Tabata mnakera

TheEngineer

New Member
Joined
Apr 6, 2016
Posts
2
Reaction score
0
Mimi ni mkazi wa tabata chang'ombe, nyumbani kwangu kuna tatizo la umeme na nimefata njia zote hapo mlizoziainisha na kujiridhisha kwamba tatizo la umeme sio INTERNAL. Cha kushangaza ni wiki sasa tangu nilipotoa taarifa emergency tabata bila msaada, kila nikipiga simu yao ya emergency wananiambia mafundi watakuja na wakifika watanipigia simu, kila siku napata shida ya kucharge simu kwa majirani kusubiri simu ambayo haipigwi.


Juzi nimeambia TB No. Walionipa imeshafanyiwa kazi wakati hakuna fundi aliyefika nyumbani, wakanipa nyingine TB No. Nyingine, lakini hadi leo sijamuona fundi yoyote.


Huu ni usumbufu sana, mimi nafanya biashara ya kuuza maziwa fresh, maziwa yote ya week iliyopita yameharibika, ya week hii nayo sina sehemu ya kuhifadhi.


Kama TANESCO wanafanya kazi kwa kujuana tuambiwe basi tujue, kama hawana hela ya mafuta waseme, au kama wengine hatuna umuhimu wa kushughulikiwa matatizo yetu watupe ruhusa tutafute fundi waje warekebishe. Sioni maana ya kuwa na kitengo emergency wakati inachukua more than a week kushughilikia tatizo moja.


Hapa ninapoishi na office za tanesco tabata ni less than 2 km, mimi nimeenda kwa mguu kutoa taarifa na sijatumia hata 1 hour kwenda na kurudi, au wanataka tuwakodie taxi hadi hapa ndo washughulikie!!?
 
Unenena vyema huku mbezi Luis ndiyo shida kabisa haipiti siku tatu lazima umeme ukatike sijui shida mini kwa Tanesco
 
We nenda ofisi ya Ilala kamuone manager mwambie aje yeye akurudishie maana wafanyakazi wake wameshindwa.Ukimkomalia hata masaa mawili hayafiki umeme utarudi
 
Aiseee Pole sana mkuu
Umeme wa tz n stress tupu
 
Back
Top Bottom