Tanesco hawana mita[luku]

Jibu gani sasa Kamanda?

Tunaumia wengine jamani!

tuwabebee bango mpaka waje hapa watueleze kinachoendelea, kwani badra masoud si ndo msemaji wao? au kazi yake ni kutoa taarifa za umeme kukatika tu. haingii akilini kuwa tanesco hawana mita, hii inaonekana kuwa simple lakini nj aibu kubwa. kama wamesbindwa kazi wafungue milango wenye uwezo wauze luku. au tukisema ni ufasadi mwingine tutakuwa tunakosea?
 
mkono mtupu haulambwi we nenda na bahasha muachie muhusika kama hajakuambia umuachie location yako itafungwa siku hiyohiyo. hiyo ndiyo hali halisi
 
Mimi nimeshahangaika mpaka nakaribia kukata tamaa!!kila siku,jibu ni meter bado hazijaja!!
Swali la kuwauliza,wanasubiri nini kuzileta?wengine bado tunatumia ile system ya kulipa kwa mwezi,na hapa naona Tanesco sasa wanatukomoa na bill za ajabu ajabu!!!!
Jamani mwenye kujua jinsi ya kutusaidia atueleze hapa jamvini!!!
 
Mkuu hata zile za deal zimeisha huku tuliko!!!


Kama ndo hivyo kwa nini basi wasitufungie umeme bila mita halafu watukadirie malipo kama tulivyokuwa tukilipa maji zamani, maana tunateseka sisi wakati hela zao za connection tumeshawalipa. ina maa=na hii serikali imeoza kila sehemu? very frustrating. utadhani nchi haina viongozi, hivi kwa nini watanzania tuna shida kiasi hiki jamani, ni laana au ni nini. maisha gani haya yani hakuna kwa kukimbilia loooh.
 
Msiendekeze kuwapa hongo ili wafanye kazi yao, mnazidi kuwaharibu maana jamaa wanajiona "Mungu watu". Kaongee nao au hata ikibidi ongea na bosi wao kuwa ushalipa kila kitu unataka huduma, the fact that hawana Luku meters isikuumize wewe mteja ambae ushakamilisha kila kitu, kwa hiyo aidha wakufungie mita ya zamani temporarily hadi watakapoleta Luku au wakuunganishe direct wakukadirie ulipe sh. ngapi kwa mwezi.... Pole sana mdau.
 
hapa issue si hongo, si wenyewe tuna tatizo hilo hilo hapa kwetu, yani tanesco hawana meter kabisa, na ni zaidi ya miezi miwili sasa.
 
sasa hela wamepokea ya nini?dawa yao ni kuruhusu makampuni binafsi ya umeme watanyooka kama ttcl
 

pole sana. Nenda tanesco muone meneja. Faster utapata meter.
 
Kumewepo uhaba mkubwa wa mita za luku hivi sasa, lkn cha ajabu tanesco wanachukua fedha za wateja kwa ahadi ya kuwapatia mita hizo, NAWAULIZA HIVI NI KWANINI TUNAWALIPA FEDHA KWA AJILI YA MITA HIZO HALI YA KUWA BADO ZINABAKI KUWA NI MALI YENU....?(WIZI) MUDA HUU MNADAI HAKUNA KWA NINI MSIRUHUSU WATU WAJINUNULIE HUKO NJE NINYI MJE MUWAFUNGIE.........?
 
Tunadhibiti ubora. Tukiwaruhusu mnunue mtachukua za kichina. Halafu baadae ikitokea shoti ikaunguza nyumba hamchelewi kuwalaumu Tanesco.
 
Hilo nalo! Kwanini tunauziwa mita na nguzo wakati zinabaki kuwa mali yao?
Huu ni wizi mwingine kwa mwananchi. Hata wabunge hawalioni hili wakalijadili bungeni¿
 
JANA gazeti hili lilichapisha habari kuhusu uhaba mkubwa wa mita za Luku ambao umelikabili Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa muda mrefu sasa kiasi cha kufanya wateja waliolipia kifaa hicho zaidi ya miezi minne iliyopita kushindwa kupata huduma hiyo. Pamoja na wateja kuahidiwa mita hizo tangu Oktoba mwaka jana, hadi hivi sasa wimbo umebaki uleule kwa upande wa shirika hilo ambalo limeendeleza ahadi zisizotekelezwa.

Ni jambo la kushangaza kuona shirika hilo limekaa kimya muda wote huo pasipo kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu kuwapo kwa uhaba huo wa Luku na ukimya huo unasemekana umeleta hofu kwa wateja na kuchochea vitendo vya rushwa kutokana na uvumi kwamba mita hizo za Luku zipo, isipokuwa zinatolewa kwa wateja wanaotoa kitu kidogo. Wateja wengi wamelalamika kwamba wamekuwa wakihangaika mara kwa mara katika ofisi za shirika hilo bila kupewa majibu ya uhakika.

Tatizo linalojitokeza hapa ni shirika hilo kufanya kazi kwa kubahatisha na kwa mazoea. Hata kauli iliyotolewa na msemaji wake juzi wakati alipoulizwa kuhusu tatizo hilo la uhaba wa mita hizo ilikuwa ya juujuu tu iliyojaa ubabaishaji. Pamoja na kukiri kwamba uhaba huo umekuwapo tangu mwaka jana, msemaji huyo alidai tatizo lilitokana na msambazaji wa shirika hilo kuchelewesha mita hizo lakini akasema zitapatikana kuanzia Ijumaa ijayo wakati zitakapoanza kutolewa kwa wateja. Hakueleza sababu zilizolifanya shirika hilo kukaa kimya muda wote huo pasipo kutoa taarifa kwa wananchi, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja.

Inasikitisha kuona shirika hilo kongwe nchini likiendelea kuendeshwa mithili ya gari bovu. Pamoja na kudekezwa na Serikali kwa kupewa kila wanachotaka, ikiwamo ruzuku na kukubaliwa kupandisha bila sababu za msingi gharama za umeme kila mwaka na kwa viwango vya juu sana, shirika hilo halionekani kusonga mbele wala kuwa na mipango ya maendeleo iliyo endelevu. Itakumbukwa kwamba, pamoja na Serikali kulikubalia kupandisha gharama za umeme mwaka huu kwa asilimia zaidi ya 40, viongozi wake hawaonyeshi ubunifu wa kulipeleka kule linakopaswa kwenda.

Katika hali ya kushangaza, viongozi wake awali walikuwa wameomba kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 155. Badala ya kubuni njia za kuongeza mapato, ikiwamo kukusanya madeni, kupambana na vishoka, kupunguza gharama za uendeshaji kwa kupunguza idadi ya wafanyakazi, shirika limeendelea kuwa tegemezi likitegemea ufadhili wa Serikali na nchi hisani pamoja na kupandisha gharama za umeme. Viongozi wa shirika hilo wameshindwa kufahamu kwamba shirika hilo haliwezi kupata mapato kama haliongezi idadi ya wateja na kwamba, ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi inahitajika idadi kubwa ya mita za Luku.

Hoja yetu hapa ni kwamba shirika hilo linashindwa kufanikiwa kwa sababu halina malengo wala dira ya kufikia malengo hayo. Ebu tujiulize, ilikuwaje mita za Luku zikaisha katika maghara pasipo wahusika kujua, wakati taratibu za ununuzi wa vifaa kama hivyo zinaeleweka? Wahusika walipaswa kujua takwimu za wastani wa mahitaji ya mita hizo kwa mwezi, miezi sita na hata mwaka mzima ili oda za manunuzi zitolewe kwa nyakati mwafaka. Ukosefu wa dira na malengo bila shaka ndicho chanzo cha utendaji kazi wa zimamoto tunaoshuhudia hivi sasa katika shirika hilo.

Tuliwahi kupendekeza huko nyuma kwamba shirika hilo livunjwe ili lisukwe upya kwa kuunda mashirika matatu ya ufuaji umeme; usambazaji umeme; na ununuzi na usambazaji wa vifaa vya umeme. Siyo siri kwamba moja ya sababu zinazokwamisha ufanisi wa shirika hilo ni muundo wake mbovu ambao umelifanya kuwa jitu kubwa mno lisiloweza kutawalika wala kuendesheka. Serikali izinduke usingizini sasa siyo tu kwa kubuni mbinu za kusuka upya jitu hili, bali pia kusimika uongozi mpya wenye dira, ubunifu na uwezo wa kufikiri.

chanzo.
Tanesco imefilisika kiasi cha kuishiwa mita za Luku?
 
kama suala ni kudhibiti ubora, toeni dokezo ni aina gani za mita zinafaa ili watu wajinunulie, aidha hakuna mtu anayependa maafa yamkute, nina imani watu watanunua mita zenye ubora pengine kushinda hizo za tanesco.
 
Nasubiri rehema za mwenyezi mungu ili na mimi nianze kuishi kwenye nyumba yenye umeme. nimeshalipa kila kitu lakini umeme sina basi yangua macho tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…