TANESCO imepoteza zaidi ya nguzo 81 kwa moto, transfoma 4 zaibiwa katika mikoa ya Iringa na Njombe. Tunajua kipindi hiki kuelekea mwishoni mwa mwaka ni kipindi cha kujiandaa na shughuli mbalimbali za kilimo Katika mikoa ya nyanda za juu kusini(Iringa na njombe).
Moja ya njia inayotumika kusafisha shamba ni kuchoma moto masalia yaliyobakia shambani baada ya kuvuna. Changamoto, miundo mingi ya TANESCO imepita maeneo ya hayo mashamba inaweza ikawa karibu na mashamba ya miti au mazao ya chakula. Sgughuli za wakulima hao uchangia Uharibifu..
Kwanini DUMA (CMS) ni mtatuzi wa changamoto hiyo? DUMA ni kwa kiswahili au CMS kwa kizungu-Corporate Management System . DUMA ni mfumo ungewezesha TANESCO Kumanage miundo mbinu yao kijeographia... Katika mkataba wa kutengeneza DUMA, Moja ya requirement ya DUMA ni kununua matumizi ya Geographical Information System, kunua Satellite imagery ya nchi nzima kama basemap, na Drones zenye quality ili kusaidia ku-manage miundo mbinu na kufanyia survey.
Kama mfumo huu ungekamilika TANESCO wangetumia satelite imagery na drones kukusanya taarifa na kutambua miundo mbinu iliyopita maeneo ya mashamba ya miti na mashamba ya kawaida . Hii ingesaidia kutatua cgangamoto za maeneo hayo ya mashambani. Kulitakiwa kuondolewa kwa nguzo zote za mbao na kuweka nguzo za cement. Nguzo za cement haziwezi kuungua na moto unaowasha wakati wa kusafisha mashamba.
Pia kuna tatizo la wizi wa transifoma , Kunapotokea matukio kama haya kunasababisha ukosaji wa huduma ya umeme. DUMA kupitia Geographical Iformation System ingewezesha TANESCO kujua ni wateja wangapi wameunganishwa katika Transifoma zilizoibiwa . Na ni wateja wa level gani ( wakaida au wakubwa), na kiasi gani cha mapato yanapotewa kutokana na wateja kukosa umeme.
Kwasasa TANESCO hawana uwezo wa kujua wateja wangapi wameunganishwa katika Transifoma A au Transfoma B.
Kama Mfumo wa DUMA ungekamilika na kutumika ipasavyo, ungewezesha TANESCO kufungua milango kwa mifumo ya Internet Of Thing (IOT) kuja kuwekeza katika TANESCO. Namaanisha SMART technology.
TANESCO LAZIMA IWEKEZE KWENYE DIGITIZATION YA MIUNDO MBINU KWA MANAGEMENT YA MIUNDO MBINU YAKE NA KUPAMBANA NA HASARA ZA MAPATO WANAYOPITIA