TANESCO imekithiri kwa vitendo visivyo vya kiutumishi

TANESCO imekithiri kwa vitendo visivyo vya kiutumishi

Mwakanshahala

New Member
Joined
Mar 31, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Wana jamvi nashindwa kuelewa kama sehemu zingine za nchi hii zinapata shida ya kuunganishiwa umeme kama Nzega haswa Nzega Mjini.

Kumekua na changamoto kubwa ya kupatiwa huduma ya maunganisho ya umeme hata baada ya kufanya malipo. Mfano mteja anafanya malipo na ndani ya miezi miwili, mitatu wakati mwingine mpka mitano hapewi huduma ya umeme.

Mteja akifatilia mara nyingi majibu ni mepesi yasioridhisha kwamba vifaa hakuna, wakati mwingine watakwambia network ya kusajili inasumbua n.k.

Lakini cha kushangaza mteja akijiongeza, namaanisha akinyoosha mkono yaani akitoa fedha kwa vijana ambao wametengeneza kama ka syndicate unafungiwa umeme ndani ya masaa machache.

Wale ambao uwezo wao ni mdogo wamekua wahanga wakubwa wa hili tatizo. Mwisho wa siku binafsi naona kama ni hujuma kwa shirika maana kupatikana kwa wateja wapya naamini ndivyo mapato ya shirika yanavyoongezeka.
 
Mbona hiyo miezi michache: kuna waliolipia wana miezi zaidi ya 6 hawajafungiwa wanasema mita hakuna lakini hajabu kuna mafremu yanajengwa na yanavyumba 10 na yanafungiwa mita....nchi hii dah... Waziri yupo wala hafatilii mikoani kuona hali halisi
 
Back
Top Bottom