TANESCO, Je mnafuta Tariff Zero?

TANESCO, Je mnafuta Tariff Zero?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Imekuwa ni kawaida kwa wale wateja ambao matumizi yao kwa mwezi ni chini ya 75 units kuwekwa kwenye tariff zero (yaani huyu mtu kwa takribani 9600/= anajipatia units 75); Sasa kuna wadau kama wanne ambao walikuwa kwenye hii Tariff nimesikia wakilalamika ndani ya kama mwezi kwamba wanaondolewa....

Hivyo kabla sijapata taarifa za uhakika siwezi kushutumu kwahio nauliza TANESCO hii ni kweli ?

Na kama ni kweli kwanini mnafanya haya mambo ya ajabu ningewaona wa maana kipindi hiki tunapopigia chapua Nishati safi mgenfanya kila mtu unit ikawa hata chini ya 100/= hapo watu wangepikia majiko ya umeme sababu kwa kufuta hii Tariff nashindwa kuwaelewa mnataka watu waanze kupikia mkaa au kutumia dollar kununua gesi ?

Tafadhali kama ni kweli hizo shutuma please rethink what you are doing....

TANESCO naomba majibu ya shutuma hizo..., hopefully sio kweli na mliowafuta ni kwamba tu mmekosea wawataarifu ili muwarudishe wakati mnapanga kutupunguzia na siwe wengine ili tuanze kutumia majiko yate ya umeme na oven (sio kuyafanya kabati)
 
Kwa taarifa nilizo nazo hiyo tarrif,zero inafutwaa kwahiyo mjiandae kisaikolojia. Wanasema inabaki vijijini Tena na wao nadhani ni kwa muda mfupi tu
 
Kwa taarifa nilizo nazo hiyo tarrif,zero inafutwaa kwahiyo mjiandae kisaikolojia. Wanasema inabaki vijijini Tena na wao nadhani ni kwa muda mfupi tu
Sijui hawa watu wana akili gani ? Hivi hii Serikali inayobinafsisha kila kitu; haitoi ajira; inahitaji pesa za nini kwenye matozo, kodi na kuomba misaada; kama kila kitu mwananchi anajitafutia..., Hio pesa inakusanywa ili ifanye nini ?

Je kupunguza bei ya umeme ili tupunguze mahitaji ya dollar ya kununua gesi kutoka nje ya nchi kipi kina faida ?
 
Daah watu mlikuwa mnafaidi!! Yaani 9000 unapata units 75? Wakati pesa hiyo hiyo mm nata unit 20
Hata hio bado ni gharama tungekuwa na maono (vision) umeme ungekuwa hata Tshs 20 kwa unit, tuna vyanzo vingi sana vya umeme potentially.., ukishakuwa na uhakika wa nishati uzalishaji utaongezeka; narudia tena kwanini watu wahangaike na kupikia gesi au so called nishati mbadala ya aina yoyote ile ?
 
Mm kinachonisikitisha wote tuko nchi moja na kiwango Cha matumizi ni kile kile kwann tarrif ziwe tofauti
 
Mm kinachonisikitisha wote tuko nchi moja na kiwango Cha matumizi ni Yale Yale kwann tarrif ziwe tofauti
Hapana kwa vijijini it made sense labda kuwapa tariff ndogo..., vilevile hii ilikuwa kwa mtu yoyote ambaye matumizi yake ni madogo (yaani hana ufujaji) sababu unajua nishati gharama unaweza ukaweka bei ya bure watu wakawa wanawasha taa hadi mchana..., hivyo wakasema kwamba mwenye matumizi machache chini ya units 75 kwa mwezi basi bei yaje inakuwa ndogo....

Ila binafsi nasema kama umeme upo wa kumwaga kwanini bei hii isiwe kwa kila mtanzania ili watu watumie umeme hata kupika na tuache kuwatajirisha wauza LPG wa nje ya nchi ?
 
Matumizi madogo ni yepi?
Chini ya Units 75 kwa mwezi ila kuna watu walichokuwa wanafanya wenyewe wakiwa hio kila mwezi ananunua kwa elfu tisa na ushee anapata 75 nyingine kwahio unakuta mtu mita yake ina units hata mia tatu kwahio kwa bahati mbaya matumizi yakizidi baadhi ya mwezi bado anakuwa anacheza mulemule....

Ila ndio hivyo nahisi hawa mabwana TANESCO kwa mijini wameondoa hio....
 
Sijui hawa watu wana akili gani ? Hivi hii Serikali inayobinafsisha kila kitu; haitoi ajira; inahitaji pesa za nini kwenye matozo, kodi na kuomba misaada; kama kila kitu mwananchi anajitafutia..., Hio pesa inakusanywa ili ifanye nini ?

Je kupunguza bei ya umeme ili tupunguze mahitaji ya dollar ya kununua gesi kutoka nje ya nchi kipi kina faida ?
Unataka utumie 9000 kupikia , na matumizi mengine mwezi mzima unaona ni sawa?
 
Unataka utumie 9000 kupikia , na matumizi mengine mwezi mzima unaona ni sawa?
Tena hio bado ni nyingi sana ukizingatia UMEME ni huduma na kuwa na Nishati ambayo bei yake sio rafiki kama nchi / kodi zetu zinalipia maradufu
  1. Uzalishaji kuwa wa gharama
  2. Kuchafua mazingira kwa watu kutumia kuni na mikaa
  3. Kutumia fedha za kigeni kununua LPG kwenye nchi nyingine wakati tuna nishati nchini
  4. Kutokutumia potential (uzalishaji ni mwingi na umeme ukizalishawa lazima utumike kutokutumia umeme at full capacity nishati hio inapotea) yaani ni kama unafungulia pipa zima la maji ili kutenga kikombe kimoja tu cha maji ya kunywa (wastage) wakati huohuo unanunua kwa jirani maji ya kunywa...
Kwahio narudia tena hata issue sio kutumia kiasi gani issue ni kwamba units bei ipungue na kama watu waliweza kutimiza mahitaji yao yote kwa 9000/= basi hio ndio Tanzania ninayoitaka mimi...
 
Hiyo bei ya umeme haipo Dunia nzima. Itakuwepo Tanzania tu
 
Hiyo bei ya umeme haipo Dunia nzima. Itakuwepo Tanzania tu
Achana na hio Bei.. Libya umeme watu walikuwa wanatumia bila kulipa (ingawa walikuwa wanatakiwa kulipa legally lakini haikuwa enforced)..., Na nchi nyingi sana ambazo zina uzalishaji mkubwa wa nishati umeme unakuwa heavily subsidized sababu faida inayopatika indirectly ni maradufu (TANESCO haipo hapo kuhakikisha inakusanya as much money as possible bali kuhakikisha inaprovide affordable electricity kwa kila mwananchi)

Pia tatizo lako unaangalia mambo kwa mafungu na sio kuangalia myororo mzima....

Tanzania nishati ni gharama na nishati ndio inatumika kwenye uzalishaji hivyo nishati kuwa na gharama vitu vyote vinapanda bei (mwananchi analipia maradufu kutokana na uzalishaji usio na ufanisi)

Tanzania ina vyanzo vyote vya kuweza kuzalisha umeme ambavyo havitumiwi to capacity; hence nishati inapotea bure..., nishati hii ikiwa tapped (bwawa tu likimaliziwa to capacity) production itakuwa double..., sasa umeme huu kwanini asitumie mwananchi na pesa yake atumie pengine kuliko pesa yako kutumika kununua dollar ili wewe umletee LPG kutoka nje ya nchi ?
 
Back
Top Bottom