Niko na changamoto hapa katika wilaya ninayotaka kuungiwa umeme. Kila kitu kimekamilika kwa upande wangu kilichobaki kutokana na maelezo ya watoa huduma wenu wanasema fomu yangu inahitajika kusainiwa ndio waje waweke umeme. Takribani wiki ya 2 sasa na inaenda 3 mhusika wakuweka sain hayupo ofisini. Nimeomba kupata maelezo hili swala linakuwaje linachukua zaidi ya wiki 3 kwakusubiri fomu yako kuweka tuu saini kisha ufunguwe umeme ukiwa kila kitu kimekamilia.Habari, Ndugu Mteja, na asante sana kwa kuwasiliana nasi.
Tunashukuru kwa ujumbe na taarifa ulizotupatia. Tumezipokea kwa ajili ya ufuatiliaji na hatua stahiki katika mikoa uliyoitaja.
Aidha, tunapenda kuwasisitiza wateja wanaokumbana na changamoto katika mchakato wa kuunganishiwa umeme kutoa taarifa kwa wakati. Mchakato wa kuunganishiwa umeme hupitia hatua na ngazi mbalimbali za kiutendaji, hivyo taarifa ya mteja ni muhimu katika kutuwezesha kufahamu hatua ambayo ombi limefikia na changamoto inayoweza kuwa imejitokeza.
Kwa hiyo, tunawahimiza wateja wenye changamoto katika mchakato huu kutoa taarifa pamoja na namba yao ya maombi, ili tuweze kufanya ufuatiliaji wa ombi husika kwa usahihi na kutoa msaada stahiki.
Tunakuomba pia uendelee kushirikiana nasi kwa kutupatia taarifa na maoni yako. Taarifa hii tumeipokea na tutaifanyia kazi katika mikoa uliyotaja kama sehemu ya jitihada za kuendelea kuboresha huduma zetu.
Asante! ^FL
Habari, Ndugu Mteja, na asante kwa kuwasiliana nasi.Niko na changamoto hapa katika wilaya ninayotaka kuungiwa umeme. Kila kitu kimekamilika kwa upande wangu kilichobaki kutokana na maelezo ya watoa huduma wenu wanasema fomu yangu inahitajika kusainiwa ndio waje waweke umeme. Takribani wiki ya 2 sasa na inaenda 3 mhusika wakuweka sain hayupo ofisini. Nimeomba kupata maelezo hili swala linakuwaje linachukua zaidi ya wiki 3 kwakusubiri fomu yako kuweka tuu saini kisha ufunguwe umeme ukiwa kila kitu kimekamilia.
Je ni uhaba wa wafanyakazi hamna ukitokea mhusika mkuu hayupo
TANESCO
Habari, ndugu mteja.Kuna viumbe huko wanaitwa Saveya aisee wanakula rushwa hao mchwa hawaoni ndani..
Asante kwa majibu yako, naomba nikuulize swali la ziada. Umeandika kuna kipindi chakusubiri wakati utaratibu wakiutendaji ukiendelea.Habari, Ndugu Mteja, na asante kwa kuwasiliana nasi.
Tafadhali fahamu kuwa baada ya kukamilisha malipo kupitia Control Number, kuna kipindi maalum cha kusubiri wakati taratibu za kiutendaji za kuunganishiwa huduma ya umeme zikiendelea. Kwa mujibu wa maelezo uliyotupatia, bado upo ndani ya muda uliowekwa kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.
Hata hivyo, ili tuweze kukupatia taarifa sahihi zaidi kuhusu hatua ambayo ombi lako limefikia na muda unaotarajiwa kuunganishiwa huduma ya umeme, tafadhali tutumie namba yako ya maombi hapa au kupitia Inbox kwa ajili ya ufuatiliaji.
Tukipokea namba yako ya maombi, tutaweza kufuatilia hatua iliyofikiwa na kukupatia mrejesho stahiki.
Asante. ^CM
Habari, ndugu mteja.Asante kwa majibu yako, naomba nikuulize swali la ziada. Umeandika kuna kipindi chakusubiri wakati utaratibu wakiutendaji ukiendelea.
Kipindi hicho ni chamuda gani? Na je hicho kipindi kablaa mteja hajaanza mchakato wowote wa umeme huwa mnampa taarifa kuwa kuna kipindi cha usubirishaji mteja anachotakiwa kusubiri.
Maelezo mengi mengi mnamaliza miti mnaleta jangwa, enzi za magu akipiga simu kwa waziri anampa wiki moja na kila kitu kinakamilika.Habari, ndugu mteja.
Kwa utaratibu wa kuunganishiwa huduma ya umeme, muda wa utekelezaji hutegemea umbali uliobainishwa kupitia tathmini ya eneo. Kwa kawaida, umbali wa hadi mita 30 huunganishiwa ndani ya siku 30, hadi mita 60 ndani ya siku 60, na umbali unaozidi mita 60 unaweza kuchukua hadi siku 90.
Tafadhali fahamu kuwa si lazima huduma ichukue muda wote uliotajwa. Mteja anaweza kuunganishiwa huduma ndani ya muda mfupi zaidi, kulingana na hatua za utekelezaji wa ombi.
Kwa kuwa ombi lako bado lipo ndani ya muda uliowekwa, tulihitaji namba yako ya ombi ili kuweza kufuatilia hatua ambayo limefikia, kulingana na matokeo ya tathmini ya eneo lako.
Aidha, kuhusu taarifa za maendeleo ya ombi, wateja hupewa taarifa na wataalamu wetu wakati wa mchakato, pamoja na wakati wa ufuatiliaji wa huduma hiyo.
Asante. ^HN
Hii ni kesi ya nyani unampelekea ngedere.Habari, ndugu mteja.
Kama unapata changamoto katika hii, tafadhali toa taaria kupitia link hii na hatua stahiki zitachukuliwa.
whistleblower.
Asante. ^CM
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.Maelezo mengi mengi mnamaliza miti mnaleta jangwa, enzi za magu akipiga simu kwa waziri anampa wiki moja na kila kitu kinakamilika.
Mmekosa nia lakini uwezo mnao na kinachohuzunisha Ni kama huyo mlaji wa mwisho anaenda kutumia bure, kumbe inawaongezea mapato.
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.
Tafadhali fahamu kuwa kuunganishiwa huduma ya umeme hufuata utaratibu unaozingatia mambo mbalimbali, ikiwemo idadi ya waombaji, upatikanaji wa vifaa, eneo husika, gharama na masuala mengine.
Hivyo, wateja hupewa muda maalum wa utekelezaji wa huduma, ambao unaweza kukamilika mapema kulingana na mazingira ya utekelezaji.
Asante. ^HN
Niulize tuu swali moja kwanini muda uwe mrefu kiasi hicho ikiwa kama mteja atakuwa na kila kitu au nyaraka zinazompatia uunganishwaji wa umeme.Habari, ndugu mteja.
Kwa utaratibu wa kuunganishiwa huduma ya umeme, muda wa utekelezaji hutegemea umbali uliobainishwa kupitia tathmini ya eneo. Kwa kawaida, umbali wa hadi mita 30 huunganishiwa ndani ya siku 30, hadi mita 60 ndani ya siku 60, na umbali unaozidi mita 60 unaweza kuchukua hadi siku 90.
Tafadhali fahamu kuwa si lazima huduma ichukue muda wote uliotajwa. Mteja anaweza kuunganishiwa huduma ndani ya muda mfupi zaidi, kulingana na hatua za utekelezaji wa ombi.
Kwa kuwa ombi lako bado lipo ndani ya muda uliowekwa, tulihitaji namba yako ya ombi ili kuweza kufuatilia hatua ambayo limefikia, kulingana na matokeo ya tathmini ya eneo lako.
Aidha, kuhusu taarifa za maendeleo ya ombi, wateja hupewa taarifa na wataalamu wetu wakati wa mchakato, pamoja na wakati wa ufuatiliaji wa huduma hiyo.
Asante. ^HN
Habari, ndugu mteja.Niulize tuu swali moja kwanini muda uwe mrefu kiasi hicho ikiwa kama mteja atakuwa na kila kitu au nyaraka zinazompatia uunganishwaji wa umeme.
Jaribuni kufikiria kwanza sasa tuko karne gani? Unadhani mteja angekuwa na option ya 2 angeweza kusubiri muda wote huo?
Hayo ni mambo mnabidi kuangalia mnawezaje boresha huduma zenu, kwa kufupisha siku za kusubiri
Habari, ndugu mteja. Pole sana kwa changamoto unayopitia.Wenzako wametufungia transformer inawaka Bure tu wakati umeme Hamna hawaja ruhusu majumbani
Habari, ndugu mteja.Anna tibaijuka alisema kadiri mnavyopanua ndio watu wanavyotamani lkn ikafurahisha watu, pelekeni huduma hata ambao hawakuwa na nia wataunga pia.
Kuna eneo fulani nje kidogo ya mkoa wa dar mzee mmoja aliwashauri wanainchi wachangie wasogeze umeme mahali walipo ilikuwa karibu nguzo karibu kumi wale wanainchi wa pwani kila siku kwao ngoma huduma za maendeleo hawawezi.
Mzee akajipinda pamoja na mikopo akagharamia kuvuta umeme hadi kwake.
baadae nyinyi mkaanza kuwaunganishia wanavijiji wengine mzee alikasirika hadi kwenda kwenye ofisi za tanesco kugomea kuwapa umeme wengine lkn mkamwambia hii ni mali ya serikali na jamii yote inapaswa kupata huduma.
yule mzee akajikuta haelewani na jamii yote iliyomzunguka na hata kufikia kusema akifa akazikwe kwao hataki kuzikwa mahali hapo.