TANESCO: Kati ya Vijiji 12,318 bado Vijiji 151 tu kufikiwa na umeme

Kadodo1

Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
25
Reaction score
24
RAIS SAMIA AMEFANYA UMEME KUWA SI ANASA- KAPINGA

๐Ÿ“Œ *Tanzania kufuta historia ya Vijiji kutokuwa na umeme

๐Ÿ“Œ Kati ya Vijiji 12,318 bado Vijiji 151 tu kufikiwa na umeme

๐Ÿ“Œ Wananchi watakiwa kutunza miundombinu ya umeme

IMG-20240816-WA0024.jpg

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amejidhatiti vyema katika kusambaza miradi ya umeme mijini na vijijini na sasa umekuwa si anasa tena kutokana na wananchi kuutumia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 16, 2024 wakati akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Mpingi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

"Ni dhamira ya Mhe. Rais kuhakikisha Vijiji vyote 12,318 nchini vinapata umeme, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), tumebakisha chini ya Vijiji 151 kuvipelekea umeme na kazi inaendelea." Amesema Mhe. Kapinga

Mhe. Kapinga ameongeza kuwa Serikali inakwenda kufuta historia ya Vijiji vya Tanzania kutokuwa na umeme kutokana na Vijiji vyote kwenda kufikiwa na nishati hiyo.

Aidha, kutokana na kuelekea kukamilika kwa upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, Kapinga amesema sasa Serikali imeelekeza nguvu katika usambazaji wa umeme kwenye Vitongoji.

Amewahakikishia Watanzania kuwa, Serikali itaendelea kupeleka huduma ya umeme katika maeneo yote nchini ili watanzania waweze kuboresha shughuli za kiuchumi.

Awali, Mha.Robert Dulle ambaye ni Msimamizi wa miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Ruvuma alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya uwepo wa umeme kwa kuunganisha kwa gharama ya shilingi 27,000 tu.

Aidha, amewaasa wananchi kutunza miundombinu ya umeme hasa kipindi cha utayarishaji wa mashamba ambapo miundombinu mingi huathirika kwa kuchomwa moto.
IMG-20240816-WA0040.jpg
IMG-20240816-WA0020.jpg
IMG-20240816-WA0022.jpg
IMG-20240816-WA0026.jpg
IMG-20240816-WA0028.jpg
IMG-20240816-WA0046.jpg
IMG-20240816-WA0050.jpg
 
Si kweli, nguzo za umeme ziko umblai mkubwa kiasi mtu wa kawaida hawezi kumudu. it is not a matter of having a supply line going over the head, what matters is the ability of poor people to be able to get connected. from a nearby Tanesco nguzo/ pole! at an affordable price
 
Futuhiiiii ndiyo ni FUTUHI.

Dar tu kuna sehemu kibao hakuna Umeme.
 
Umeme kwa wote safi sana.
Kupata Kwa hiyo Bei ya 27,000 viijijin ni shida .ukiomba kufuniea nyumbani Takukuru na CAG waende kukagua je wanavijiji wangapi waliomba kugungiwa umeme na lini waliomba na Kwa Nini Hadi Leo hajapewa control number walipie hiyo Hela wafungiwe umeme

Wataona maajabu

Au serikali iombe serikali za vijiji zipeleke majina ya wote ambao waliomba kufungiwa umeme na hawajafungiwa

Kuna madudu balaa kisingizio nguzo
 
Hongera kwa Tanesco kwa kusambaza umeme nchi nzima
Umeme umefika vijijini lakini wanavijiji wengi haujawafikia majumbani sababu ya rushwa na ukiritimba.Nguzp za umeme zomefika vijijini lakini wanakijiji wengi Bado kupata majumbani mwao

Wizara ianzie operation ya kufungia umeme Sasa watu majumbani vijijini kitaifa wayangaze kabisa kuwa wiki Fulani itakuwa ya operation fungia umeme majumbani Kwa wanakijiji wote walioomba
 
Waziri mpya changamoto ya kwanza hiyo watu vijijini wanaomba umeme hawafungiwi.wakati wako tayari kulipa hiyo elfu 27000
 
RAIS SAMIA AMEFANYA UMEME KUWA SI ANASA- KAPINGA

๐Ÿ“Œ *Tanzania kufuta historia ya Vijiji kutokuwa na umeme

๐Ÿ“Œ Kati ya Vijiji 12,318 bado Vijiji 151 tu kufikiwa na umeme

๐Ÿ“Œ Wananchi watakiwa kutunza miundombinu ya umeme

View attachment 3071910
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amejidhatiti vyema katika kusambaza miradi ya umeme mijini na vijijini na sasa umekuwa si anasa tena kutokana na wananchi kuutumia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 16, 2024 wakati akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Mpingi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

"Ni dhamira ya Mhe. Rais kuhakikisha Vijiji vyote 12,318 nchini vinapata umeme, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), tumebakisha chini ya Vijiji 151 kuvipelekea umeme na kazi inaendelea." Amesema Mhe. Kapinga

Mhe. Kapinga ameongeza kuwa Serikali inakwenda kufuta historia ya Vijiji vya Tanzania kutokuwa na umeme kutokana na Vijiji vyote kwenda kufikiwa na nishati hiyo.

Aidha, kutokana na kuelekea kukamilika kwa upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, Kapinga amesema sasa Serikali imeelekeza nguvu katika usambazaji wa umeme kwenye Vitongoji.

Amewahakikishia Watanzania kuwa, Serikali itaendelea kupeleka huduma ya umeme katika maeneo yote nchini ili watanzania waweze kuboresha shughuli za kiuchumi.

Awali, Mha.Robert Dulle ambaye ni Msimamizi wa miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Ruvuma alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya uwepo wa umeme kwa kuunganisha kwa gharama ya shilingi 27,000 tu.

Aidha, amewaasa wananchi kutunza miundombinu ya umeme hasa kipindi cha utayarishaji wa mashamba ambapo miundombinu mingi huathirika kwa kuchomwa moto.
View attachment 3071911View attachment 3071912View attachment 3071913View attachment 3071914View attachment 3071915View attachment 3071917View attachment 3071918
Uongo mkubwa!
 
  1. RAIS SAMIA AMEFANYA UMEME KUWA SI ANASA- KAPINGA

๐Ÿ“Œ *Tanzania kufuta historia ya Vijiji kutokuwa na umeme

๐Ÿ“Œ Kati ya Vijiji 12,318 bado Vijiji 151 tu kufikiwa na umeme

๐Ÿ“Œ Wananchi watakiwa kutunza miundombinu ya umeme

View attachment 3071910
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amejidhatiti vyema katika kusambaza miradi ya umeme mijini na vijijini na sasa umekuwa si anasa tena kutokana na wananchi kuutumia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 16, 2024 wakati akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Mpingi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

"Ni dhamira ya Mhe. Rais kuhakikisha Vijiji vyote 12,318 nchini vinapata umeme, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), tumebakisha chini ya Vijiji 151 kuvipelekea umeme na kazi inaendelea." Amesema Mhe. Kapinga

Mhe. Kapinga ameongeza kuwa Serikali inakwenda kufuta historia ya Vijiji vya Tanzania kutokuwa na umeme kutokana na Vijiji vyote kwenda kufikiwa na nishati hiyo.

Aidha, kutokana na kuelekea kukamilika kwa upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, Kapinga amesema sasa Serikali imeelekeza nguvu katika usambazaji wa umeme kwenye Vitongoji.

Amewahakikishia Watanzania kuwa, Serikali itaendelea kupeleka huduma ya umeme katika maeneo yote nchini ili watanzania waweze kuboresha shughuli za kiuchumi.

Awali, Mha.Robert Dulle ambaye ni Msimamizi wa miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Ruvuma alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya uwepo wa umeme kwa kuunganisha kwa gharama ya shilingi 27,000 tu.

Aidha, amewaasa wananchi kutunza miundombinu ya umeme hasa kipindi cha utayarishaji wa mashamba ambapo miundombinu mingi huathirika kwa kuchomwa moto.
View attachment 3071911View attachment 3071912View attachment 3071913View attachment 3071914View attachment 3071915View attachment 3071917
Uongo huu fresh tu.
Ngoja niongezee mwingine:

1. Maji safi na salama yanapatikana kila siku, mjini na vijijini, kwa asilimia 97 za kaya zote nchini.Fresh tu

2. Kabla ya June 2025, Tanzania itarusha satellite zake mbili na kutuma chombo kimoja cha upelelezi mwezini.
 
Si kweli, nguzo za umeme ziko umblai mkubwa kiasi mtu wa kawaida hawezi kumudu. it is not a matter of having a supply line going over the head, what matters is the ability of poor people to be able to get connected. from a nearby Tanesco nguzo/ pole! at an affordable price
very nice, suala la umeme ni changamoto sana haswa kwa sisi raia wa kipato cha chini, hivi mkulima wa kawaida ambaye anao uwezo wa kulipa bill kuanzia elfu 5 hadi kwa mwezi tu unamwambie atoe milioni tano kufikishiwa umeme kwakwe itawezekana kwakk, kwanini serikali isimfikishie umeme alafu ikawa inalipisha kwa kukata pesa kidogo kidogo
 
ANATAPANYA HELA KWENYE MIPIRA, kIZIMKAZI NA UPUUZI KAMA HUO
 
Milions of money wanazowekeza kununua mi dege inayotia hasara taifa kila mwaka wangewasambazia umeme watu kwa mkopo ikawa kila mwezi wanakata elfu kumi tu kupitia luku kwa muda fulani nadhani wangevuna pesa ya kutosha na wakati huohuo wakiboresha maisha ya wananchi, SERIKALI YETU INAKOSA WATU WENYE MAONO
 
Back
Top Bottom