TANESCO kuna Hitilafu ya Manunuzi ya LUKU kupitia njia za mitandao ya simu na Benki. Wataalamu wa GePG wanashughulikia

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawajulisha wateja wake kuwa kumetokea changamoto ya manunuzi ya umeme (LUKU) hali inayosababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia njia za mitandao ya simu, mawakala pamoja na njia za kibenki.

TANESCO kupitia wataalamu wake imejiridhisha kuwa changamoto hii inasababishwa na hitilafu kwenye Mfumo wa Malipo ya Serikali (GePG).

Tayari wataalamu wa GePG wanashughulikia changamoto iliyojitokeza ili huduma iweze kurejea katika hali ya kawaida.

TANESCO inatoa wito kwa wataalamu wa GePG kushughulikia jambo hili kwa umuhimu mkubwa ili kuwaondolea wateja usumbufu na kushindwa kufanya manunuzi ya umeme kunakosababishwa na changamoto hiyo.

Shirika litawafahamisha wateja wake huduma zitakapoperejea kikamilifu.

​
 
Ok! Jana tumepata Sana changamoto. Angalau leo Hali imetulia.
 
nawapongeza wataalamu..

CCM hoye!,chama cha mapinduzi kidumu milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…