Hivi karibuni Tanesco imeanzisha utaratibu mpya wa kusoma matumizi ya umeme katika mita kutokea makao makuu Dar. Mita mpya zilizowekwa huwa juu sana katika mlingoti wa umeme ambayo mtumiaji hawezi akajua ametumia umeme kiasi gani tofauti na zamani ambayo mtu angeweza soma kiasi alichotumia. Tanesco inachofanya ni kutuma kila mwisho wa mwezi bill ambayo mlaji huwezi kujua kama ni bill halali. maana yake huwezi kuague kabisa lako ni kulipa. Je mlaji anajuaje kuwa ametumia kiasi hicho? Nadhani tunaweza kuibiwa.